Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Alert: Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya ajiengua CCM

milya Taarifa za kuaminika zilizotapakaa katika viunga mbali mbali vya jiji la Arusha, hususani kwa wanaofuatilia siasa za nchi hii zinaeleza kuwa James Ole Milya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoani Arusha ametangaza kujiengua katika chama chake hii leo asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, James ameongea na waandishi wa habari na wananchi kupitia Radio 5 ya Arusha, na kueleza hatua yake hiyo ya kujitoa katika chama chake cha CCM na kujiunga na CHADEMA.

Mwenyekiti huyo, ametangaza kujiuzuru nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa  kwa madai kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.

Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini Arusha. Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.

Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

ALisema kuwa inasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.

Millya alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kw anamna moja au nyingine na kauli hiyo.

Aidha alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kwamatumaini kama muathirika wa Ukimwi.

Hata hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.

Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi sasa, aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru, ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili ya ukombozi wa kweli. Millya hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa Afrika Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichinjiwa baharini na kutolewa jina lake.

Wakati Kiongozi huyo akitangaza kuachia ngazi hiyo ya juu ya UVCCM, ndani ya Chama cha CCM, Mkoa wa Arusha, Vijana mbalimbali wameonekana kutoamini walichosikia na wengi wao wakionyesha nia ya kumfuata.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanahusisha uamuzi wake huu na kuondolewa kwake katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO