Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwenyekiti wa CHADEMA Arumeru Mashariki auawa kwa kuchinjwa shingo

RSCN0033

Aliekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa-River, Arumeru Mashariki Ngd Msafiri Mbwambo (38) kabla ya kifo chake

Furaha ya wafuasi wa CHADEMA Kata ya Usa River, Arumeru waliokuwa wakifuatilia ushindi wa Mh Tindu Lissu (hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wake jana)kupitia taarifa ya habari ya saa mbili jana usiku iligeuka kuwa majonzi baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa CHADEMA katika Kata hiyo.

Mwenyekiti huyo, Ndg Msafiri Mbwambo alifikwa na mauti baada ya kukatwa shingoni na kitu chenye makali kutokea upande wa nyuma wa shiongo kuja mbele. Wahusika wa tukio hilo bado hawajajulikana na Polisi wamekwishaanza upelelezi.

Hata hivyo, hisia za wananchi wengi waliohuzunishwa na kifo hicho cha kikatili zinahusisha tukio hili na hasira na chuki za kisiasa.

Majirani wa marehemu wanaeleza kuwa kabla ya kufikwa na mauti, marehemu alikuwa na mke wake wakiwa duka fulani (kwa Hashimu) wanakuywa soda.  Mara akapigiwa simu na mtu ambae alimtaka wakutane mahali fulani. Akamuaga mke wake na kuelekea alikoitwa lakini hakuweza kurudi tena. alikuwa amefuata kifo chake mwenyewe bila kujua.

Marehemu aliuliwa sehemu ya wazi jirani na makazi ya watu katikati ya barabara eneo maarufu Kwa Kisambale, jirani na uwanja wa mpira. Majirani na eneo la tukio waliokuwa wa kwanza kumuona wanasema walikmuta bado hajakata roho, mguu mmoja bado uko juu ya pedeli ya pikipiki yake, huku mifuko yote ya nguo ikiwa nje kuashiria kuwa ilipekuliwa.

Waliofanya mauaji hayo waliondoka na simu yake na vitu vingine lakini pikipiki na ufunguo wake waliviacha.

Marehemu Mwambo alikuwa ni nguzo kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Katani kwake kama Mwenyekiti na alitoa mchango mkubwa sana kufanikisha ushindi wa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari (CHADEMA) katika uchaguzi uliofanyika majuma matatu yaliyopita, Aprili 1, 2012.

msafiri achinjwaJinsi marehemu alivyochinjwa. Ni ukatili wa hali ya juu kwa binadamu

Mwandishi wa taarifa hii alifanya mahojiano na viongozi wenzake katika Kata pamoja na majirani wanaomfahamu na wote wameeleza marehemu hakuwa mtu wa ugomvi, hakuwa mnywaji wa pombe. Alikuwa ni kijana mtulivu na mtu wa watu.

Marehemu alikuwa anajishughulisha na ufundi ujenzi wa nyumba ambapo alikuwa akipokea tenda za watu mbalimbali kuwajengea.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Usa River (Leganga) na kuna Kamati ya chama ngazi ya Kata imeundwa kusaidiana na ndugu wa marehemu. Kamati hiyo inaongozwa na Ndg Nuru Maeda, Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Magadirisho ambae alinusurika kifo wakati wa kampeni za mwezi Machi mwaka huu baada ya kutekwa na watu wasiojulikana katika maswala ya siasa.

Mwili wa marehemu ilikuwa usafirishwe kesho kwenda Same kwa maziko lakini Mbunge wa Arumeru Mashariki na viongozi wengine wa Chama Mkoa waliomba safari hiyo ifanyike keshokutwa Jumatatu ili kuruuhsu uchunguzi wa kidaktari uweze kufanyika kwanza.

Marehemu ameacha mke na watoto.

Aidha, taarifa nyingine zinaeleza kuwa Katibu wa CHADEMA katika  Kata hiyo, Ndg Saidi Pilikwela pamoja na vijana wengine waliokuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za chadema, wamedai kupokea meseji za vitisho kutoka kwa watu wanaoafahamu, hali inayaowafanya waishi kwa wasiwasi na mashaka makubwa.

Blog hii inawapa pole wafiwa wote, na Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema!!

Marehemu Msafiri Mbwambo enzi za uhai wake. Hapa ilikuwa ni Bungeni Mjini Dodoma alipoenda kumsindikiza Mbunge wake Joshua Nassari mapema mwezi huu.

DSCN0026Baadhi ya wananchi, wanachama na viongozi wengine wa CHADEMA Kata ya Usa-River wakijadiliana utata wa kifo cha Mwenyekiti wao, ndani kikao kinaendelea kupanga mipango ya mazishi na msiba kwa ujumla.

DSCN0041Wananchi wakishangaa kwa majonzi, sehemu ambapo marehemu alichinjwa kama kuku na damu kutapkaa chini kama picha inavyoonesha

DSCN0035Hii ni nyumba ya marehemu alikuwa hajaimalizia kwa ajili ya wapangaji. Nyumba yake ya kuishi iko nyuma ya hii (haionekani)

Bendera ya chama (CHADEMA) ikipepea nusu mlingoti mbele ya Ofisi ya Kata User-River . Hali ni ya majonzi sana..

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO