UONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, jana ulitoa tamko la kumsafisha aliyekuwa Mwenyekiti wake, James Ole Millya dhidi ya tuhuma za kuondoka na Sh2 milioni zilizokusudiwa kuanzisha Saccos na kutoa onyo kwa wanachama na viongozi wake mkoani hapa kuacha mara moja tabia ya kila mmoja kujitolea taarifa atakavyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdallah Mpokwa alisema tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mwenyekiti wake wa zamani ni za upotoshaji.
Katika hali iliyoonekana kama CCM na Umoja huo mkoani Arusha kutaka kufunga mjadala wa Ole Millya aliyehamia Chadema, Mpokwa alisema tangu alipohamishiwa Arusha hakuwahi kupata kumbukumbu wala taarifa zozote za fedha zinazoonyesha kuwa aliyekuwa mwenyekiti huyo aliondoka bila kukabidhi.
Ckick here to read full story on Mwananchi, 25th April 2012
0 maoni:
Post a Comment