Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uharibifu wa tabaka la ozoni waleta madhara

na Evelyn Mkokoi, wa Tanzania Daima (Arusha)

KUONGEZEKA kwa magonjwa ya saratani ya ngozi, uharibifu wa macho maarufu kwa jina la mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi, kumeelezwa kusababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa tabaka la ozoni.

Hali hiyo inaelezwa kuwa inatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira.

Hayo yalielezwa jana mjini hapa katika hotuba ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi mchundo wa majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala, iliyosomwa na Ofisa Mazingira wa Mkoa, Julius Achiula, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa.

Alibainisha kuwa baadhi ya kemikali hizo ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipoozi katika mafriji, viyoyozi, vifaa vya kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.

Uhifadhi wa tabaka la ozoni umetokana na utekelezaji wa mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania ni mwanachama.

Warsha hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, imehusisha washiriki kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Chuo cha Ufundi Veta Moshi, wanahabari, maofisa mazingira wa Mkoa wa Arusha na mafundi mchundo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO