Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM ni Mzigo Kwa Taifa, Nimejiengua na Wengi Watanifuata– Ole Millya

James-Ole Aliekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Arusha, James Ole Millya amesema Chama Cha Mapinduzi ambacho alitangaza kukihama jana, ni mzigo kwa taifa.

Kauli hiyo ameitoa leo asubuhi wakati akizungumza katika kipindi cha “Morning Jam” kupitia Capital Radio Fm ya Jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi hicho ambacho kilikuwa na mada inayosema “Viongozi wa vyama vya siasa kuendelea ‘kujivua gamba’ kuna ishara gani kwa siasa za Tanzania?”, Millya aliongea mambo mengi kuhusiana na uamuzi wake wa kujitoa CCM na kutangaza nia ya kujiunga na wapinzani wakuu wa CCM nchini kwasasa, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Katika maelezo yake, Millya anashangaa wanaomtuhumu kuwa amejivua gamba ilhali falsafa ya ‘kujivua gamba’ ilibuniwa ikilenga viongozi wa serikali waliopotoka kimaadili hasa kwa kuhusishwa na masuala ya rushwa, maswala ambayo amekana kuwahi kuhusia kwala kutuhumiwa nayo.

Kupitia mazungumzo yake hayo leo, ameitahadharisha CCM na viongozi wake kuwa watambue mabadiliko yanayoendelea kote duniani kwasasa hayatakiacha salama chama chake hicho cha zamani.

“Mabadiloko mengi yanatotokea sasa ulimwenguni, CCM isiamini kwamba hayatatokea na hapa. Huu ni wakati wa mbadiliko. Mimi nimeanza (kujiengua CCM) lakini wengi watanifuata” alisema Millya

Aidha, alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi kujua kama tayari ameshajiunga rasmi na CHADEMA, Ole Millya alisema yuko kwenye taratibu za kujinga na chama hicho lakini dhamira yake kwa sasa ni kuendelea kuwatumikia watanzania kupitia CHADEMA.

“Niko kwenye taratibu (za kujiunga na CHADEMA), nimeshaamua na moyo wangu uko CHADEMA. Sababu ninazo na CHADEMA ndio ‘interest yangu’. Nimeamua kuendelea kuwatumikia watanzania, nitaamini falsafa ya CHADEMA, nitaheshimu viongozi wa CHADEMA” alisema James Ole Millya

Baadhi ya wasikilizaji wa kipindi waliopewa nafasi kutoa maoni yao kuhusiana na mada husika ya kipindi hicho kwa siku ya leo, walisema mfululizo huu wa viongozi wa CCM ‘kujivua gamba’ unatoa picha na tafsiri kwamba yapo mabaya zaidi yaliyojificha ndani ya CCM na kupitia matukio kama haya ndipo wanapoweza kuyagundua.

Wasikilizaji wengine walihoji kwanini James Ole Millya asemwe vibaya na viongozi wa chama alichokiama kipindi hiki baada ya kujitoa na sio akiwa mwanachama na kiongozi mwenzao, na kueleza kwamba kama alikuwa mzigo kwa chama walishaindwaje kumuondoa muda wote huo, na hawakuwahi kusema hayo mabaya yake ndani ya chama hadi alipoamua kujiengua mwenyewe.

Kabla ya kutangaza kujiengua CCM jana, James Ole Millya alikuwa anashikilia nafasi muhimu za uongozi katika chama hicho ikiwemo uenyekiti wa vijana wa CCM Mkoani Arusha.

Nafasi nyingine alizoachia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa, na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

Huu ni mwelekeo mwanana kwa itikadi thabiti za CHADEMA,uozo uliopo katika hiki chama kinachowahadaa Watanzania!,waso dira juu ya mstakabari wa taifa la kesho.Hongera Millya tuliendeshe gurudumu la harakati kwa ukombozi wa taifa letu.Umefanya uamuzi sahihi kujiunga na CHADEMA kwani wote ni watetezi wa haki tofauti na siasa za uzushi,danganya toto,vitisho na upindishwaji wa sheria kama inavyoshuhudiwa kwa sasa.Sisi kama vijana na wafuasi wa CCM KUiacha na kuwa wanaharakati wa kutetea haki kwa maendeleo ya vijana hapo baadaye.

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO