Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Walioenguliwa UVCCM Mbeya kutoa msimamo

VIONGOZI wa Umoja wa Vijana na Chama cha Mapinduzi (UVCCM), waliovuliwa uongozi na Baraza Kuu la Vijana Mkoa wa Mbeya, wanatarajia kujibu mapigo kwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho, zimesema kuwa baada ya baraza hilo kumvua nafasi ya ukamanda wa UVCCM mkoa, mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya, Stephen Mwakajumilo na Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Onesmo Nswilla, sasa vita kali imeanza.

Nswilla anatarajia kuzungumzia sakata hilo mbele ya waandishi wa habari na kutoa dukuduku lake.

Alipotafutwa kwa njia ya simu na Tanzania Daima ili kuthibitisha tetesi hizo, Nswilla alikiri kuwepo kwa mpango huo akisema kuwa atazungumzia hatima ya uongozi wake na mengine mengi.

Chanzo: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO