Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Moto wateketeza Maduka 8 ya biashara Jijini Arusha leo

Zaidi ya ‘frame’ 8 za wafanya biashara katika kona ya Mtaa wa Livingstone na Wasangu, eneo maarufu kama Chini ya Mti, Kata ya Levolosi, Arusha zimeteketea kwa moto mchana wa leo.

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda, moto huo unaelezwa kuanza majira ya saa saba mchana kwa kuanza na sehemu ndogo ya vinywaji katika jengo lenye maduka hayo na baadae kusambaa maeneo mengine kwa kasi ya ajabu.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana, na wala jumla ya hasara iliyosababishwa na moto haijaweza kupatikana…lakini inahisiwa moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Diwani wa Levolosi (CHADEMA) Mh Ephata Nanyaro alisema kilichosababisha madhara ya moto kuwa makubwa ni kitendo cha Kikosi cha Zimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio wakiwa kamilifu pamoja na kwamba walipewa taarifa mapema.

Maduka yaliyoathirika na mto huo yalikuwa ni ya spea za magari na vyombo vingine vya moto, nguo, vipodozi na urembo.

Mengine ni maduka ya majokofu, redio na vifaa vingine vya kelektroniki.

Moto huo uliweza pia kuathiri sehemu ya Msikiti wa Masjid Ahmad (Ahmadiyya Muslim Jamaat Arusha) uliopo jirani na maduka hayo..

moto Arusha

DSCN0046  Wananchi wakishangaa uharibifu uliotokana na moto huo

DSCN0045

DSCN0042 Duka mojawapo la spea za magari likiwa limeteketea kabisa na kila kilichokuwamo ndani

DSCN0043

DSCN0044

Picha zote na Tumainiel Seria!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO