Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Joshua Nassari (Mb) awa kivutio mechi ya Oljoro na Yanga Mjini Arusha leo

DSCN9995Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu waliofurika katika uwanja wa Kumbukumbu ye Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha kushuhudia mpambano baina ya timu za Oljoro ya Arusha na Yanga ya Dar es Slaam, Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom. Matokeo ya mchezo huo yalikuwa Oljoro 1 – 4 Yanga.

DSCN9996Hapa Mh Nassari yupo jukwaa la mashabiki wa Simba wakipiga stori huku wanatazama mpambano

IMG00133

Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh Mulugo. Kabla ya kuchangamana na mashabiki, Mh Nassari alifika viwanjani hapo na kwenda Jukwaa kuu kusalimiana na viongozi wengine na kisha akashuka na kuelekea jukwaani kwa mashabiki. Baadae baadhi ya mashabiki waliogundua yupo uwanjani pale ‘wakapiga kelele’ akawatembelee, hatua iliyomlazimu kuhama jukwaa moja baad ya jingine na kusalimiana nao. Baadhi ya mashabiki walishindwa kufuatilia mpambano kwa makini na kuishia kumshangaa Mbunge huyo mpya ambae kwa sasa analazimika kuhudumia kiuwakilishi watu wake wa Arumeru na wa Arusha Mjini kufuatia Mahakama Kuu Arusha kutengua ubunge wa aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema (CHADEMA).

Picha zote na SERIA Jr

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO