Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uteuziwa wa wagombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

bu1

(Inatolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 5(3) ya Nyongeza ya Pili  ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007)

_______________________________

1.0 Tarehe 9 Machi, 2012 nilitoa Tangazo kwa vyombo vya habari na gazeti la Serikali juu ya  kuwepo kwa nafasi Tisa wazi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kufuatia kufikia ukomo wa maisha ya Bunge la sasa hapo 04 Juni, 2012.

Katika Tangazo hilo niliwaomba wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo wafanye mchakato wa kugombea kupitia vyama vyao vya Siasa na fomu za wagombea waliopendekezwa zirejeshwe Ofisi ya Bunge kabla ya saa 10.00 jioni tarehe 10 Aprili, 2012 ambayo ndiyo siku ya uteuzi.  Jumla ya Wagombea 34 kutoka Vyama vya Siasa vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP na TADEA wamerudisha Fomu.

2.0 Zoezi la uteuzi limekamilika, Wajumbe 33 wametimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, hivyo, wameteuliwa kugombea nafasi hizo.   Aidha, Mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya  kuthibitisha uraia wake na kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 5(3) na 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge, hivyo hakuteuliwa kugombea.

Ifuatayo ni Orodha ya Wagombea walioteuliwa na wasioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki:-

1. WAGOMBEA WALIOTEULIWA

KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE

1. Nd. Angela Charles Kizigha - CCM

2. Nd. Fancy Haji Nkuhi - CCM

3. Dkt. Godbertha Kokubanza Kinyondo - CCM

4. Nd. Janet Deo Mmari - CCM

5. Nd. Janet Zebedayo Mbene - CCM

6. Nd.  Maryam Ussi Yahya - CCM

7. Nd. Rose Daudi Mwalusamba - CUF

8. Nd. Sebtuu Mohamed Nassor - CCM

9. Nd. Shy-Rose Sadruddin Bhanji - CCM

10. Nd. Sofia Ali Rijaal - CCM

KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR

1. Nd. Abdullah Ali Hassan Mwinyi - CCM

2. Dkt. Ahmada Hamad Khatib - CCM

3. Dkt. Haji Mwita Haji - CCM

4. Nd. Khamis Jabir Makame - CCM

5. Dkt. Said Gharib Bilal - CCM

6. Nd. Zubeir Ali Maulid -CCM

KUNDI C: WAGOMBEA WA VYAMA VYA UPINZANI

1. Nd. Antony Calist Komu - CHADEMA

2. Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha - UDP

4. Nd. Juju Martin Danda - NCCR-MAGEUZI

5. - Nd.  Micah Elifuraha Mrindoko - TLP

6. Nd. Mwaiseje S. Polisya - NCCR-MAGEUZI

7. Nd. Nderakindo Perpetua Kessy - NCCR- MAGEUZI

8. Nd. Twaha Issa Taslima - CUF

KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA

1. Nd. Adam Omar Kimbisa - CCM

2. Nd. Bernard Musomi Murunya - CCM

3. Nd. Charles Makongoro Nyerere - CCM

4. Dkt.  Edmund Bernard Mndolwa - CCM

5. Nd. Elibariki Immanuel Kingu - CCM

6. Dkt. Evans Mujuni  Rweikiza - CCM

7. Nd. John Dunstan Lifa-Chipaka - TADEA

8. Nd. Mrisho Mashaka Gambo - CCM

9. Nd. Siraju Juma Kaboyonga - CCM

10. Nd. William John Malecela - CCM

2.      MGOMBEA AMBAYE HAKUTEULIWA

1. Nd. Mohamed Abdulrahman Dedes - CUF

3.1    Hivyo, bila ya kuathiri shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge, tarehe 17 Aprili, 2012 saa Nne na nusu asubuhi au muda mfupi baada ya hapo nitawasilisha  majina ya Wagombea kwa wapiga kura.

Napenda kutoa shukrani kwa Wagombea wote kwa ushirikiano wao katika kukamilisha zoezi hili la uteuzi.  Aidha, tunawaomba wapiga kura, wakati utakapofika, wazingatie matakwa ya Sheria na Kanuni zinazotawala chaguzi hizi.

Imetolewa na:

Dkt. Thomas D. Kashililah                                                               

KATIBU WA BUNGE NA                                                                       

MSIMAMIZI WAUCHAGUZI

BUNGENI DODOMA

14 APRILI, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO