Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Bayern Munich 2 - 1 Real Madrid, UEFA Champions League 2012 (first leg –Semi-Final)

Bayern_Munich_y_Real_Madrid_large

Game imepigwa uwanja wa Allianz Arena mjini Munich usiku huu na matokeo ndio hayo

Wafungaji wa mechi hii ni  Frank Ribbery alieipatia Bayern Munich bao la kwanza dakika ya 17 baada ya kutokea piga nipige iliyotokana na mpira wa kona na kumkuta mfungaji alieachia shuti la moja kwa moja hadi wavuni.

Goli la pili na la ushindi kwa bayern lilifungwa na Mario Gomez alieandika goli la ushindi kwa timu yake dk ya 90, zikiwa zimesalia dk 3 tu mpira kumalizika baada ya kupokea krosi nzuri ya Arjen Roben kutokea upande wa kulia mwa uwanja..

Real Madrid walijipatia bao la kufutia mchazi dakika 8 baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia  kwa Mesut Ozil. Bao hilo lilipatikana baada ya Christiano Ronaldo kukusa nafasi ya wazi akiwa amebaki yeye na kipa na kisha kupiga mpira uliombabatiza golikipa miguuni na kurudi uwanjani. Hata hivyo rebound hiyo ilinaswa na Karim Benzema ambae alimpasia Ronaldo tena liaekuwa pembeni katibu na goli na kuingiza krosi ya haraka iliyomaliziwa na Angel di Maria kwa uzuri kabisa.

Matokeo haya ni pigo kwa “The Special One” na bila shaka ataenda kujipanga kwa mpambano wa marudio. Kesho kutakuwa na mpambano mwingine wa kukata na shoka baina ya Chelsea ya Uingereza chini ya kocha wa muda Di Mateo na Barcelona ya Hispania iliyo chini ya kiungo wake mchezeshaji wa zamani Pep Guardiola.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO