Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM yajikanyaga kuhusu jimbo la Arusha Mjini

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakiwezi kurudisha jimbo la Arusha Mjini kutokana na kauli zilizokuwa zinatolewa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema ambazo zinaenda kinyume na kanuni na sheria za uchaguzi.

Kauli hiyo imekuja katika kipindi kifupi baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema kwa madai ya kutoa lugha za matusi, kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Batilda Buriani ambaye aligombea kwa tiketi ya CCM.

Shauri hilo namba 13/2010 lilifunguliwa na wapiga kura watatu, Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo wanaowakilishwa na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida ambao kwa pamoja wanadai Lema alitoa lugha hizo dhidi ya mgombea huyo.

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema kuwa, licha ya Lema kuwasumbua katika kipindi chote cha uchaguzi na ubunge wake, hawezi kushinda hata akisimama kwa mara nyingine.

“Lema mtoto wa mjini kweli kweli, aliweza kutusumbua tangu kwenye kampeni hadi kwenye kipindi cha ubunge, lakini sasa hivi hata akisimama tena hawezi kushinda, kwa sababu amekiuka sharia na taratibu za kanuni za uchaguzi,” alisema Chatanda.

Aliongeza kutokana na hali hiyo chama hicho kimejipanga upya ili kuhakikisha kuwa jimbo hilo linarudi mikononi mwao jambo ambalo litaweza kuwavunja nguvu wanachama wa Chadema mkoani humo.

Alisema CCM iko makini licha ya kuwepo kwa tofauti za hapa na pale ambazo zimeweza kuwaondoa baadhi ya wanachama wa chama hicho mkoani humo, lakini ni mwendelezo wa kuwaondoa wanachama wanaokwenda kinyume na sharia za chama chao, jambo ambalo limewafanya baadhi yao kujiondoa wenyewe.

“Sio hao tu, kuna wengine nao wako njiani wanaweza kuondoka wakati wowote, lakini mkakati wetu utabaki pale pale, ni kuhakikisha kuwa, majimbo ya CCM ya mkoa wa Arusha ambayo yamechukuliwa na upinzani yanarudi,” aliongeza.

Published by Mwananchi, 28th April 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO