Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mahakama Kuu Arusha Yamvua Ubunge Gobless Lema

KATIKA Hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Bw
Goodbless Lema ametenguliwa na Mahakama Kuu kanda ya Arusha katika
matokeo yake ya Ubunge  na kisha Mahakama hiyo kutangaza hadharani
siyo mbunge

Akisomewa hukumu hiyo  mapema leo na Jaji Mfawidhi kutoka katika kanda
ya Sumbawanga, Jaji Gabriel Rwakabirira alisema kuwa ameridhika na
ushahidi wa pande zote mbili na ndio maana ametoa hukumu.

Jaji Gabriel alisema kuwa alipokea dondoo 10 kutoka kwa wafuasi wa CCM
ambapo alifanikiwa kukubali dondoo 8 na kisha kukutaa dondoo nyingine
mbili kwa mujibu wa sheria na taratibu za Mahakama.

Alisema kuwa Mbunge Lema alitenda makosa hayo kati ya mikutano 60
ambayo aliifanya katika kipindi cha kampeni za mwaka 2010 ambapo
alimchafua mshindani wake mkuu, Dkt Batilda Burian kinyume cha
sheria

Jaji huyo alifafanua kuwa mbunge huyo alikutwa na makosa nane hali
ambayo inamfanya mpaka sasa angatuke kwenye ubunge kwa mujibu wa
sheria na taratibu za Mahakama.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa anamuagiza msajili wa Mahakama kwa
kanda ya Arusha kuhakikisha kuwa anapeleka taarifa kwa tume ya
uchaguzi juu ya kuenguliwa kwa Mbunge huyo lakini bado yuko huru
kukata rufaa hata kwa ngazi za juu sana.

Awali aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Arusha Mjini Goodbless
Lema,aliwaambia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika katika  viwanja
vya Mahakama hiyo kuwa bado yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa
hali hiyo atashinda tu

Lema alisema kuwa kitu kilichofanyika katika Mahakama hiyo na kisha
kutengua ubunge wake kiinaonesha wazi jinsi Mahakama isivyoweza
kutumia demokrasia na hali hiyo kama itaendelea ni wazi kuwa masikini
watakosa haki zao za msingi

Lema aliwaambia wannachi wa jimbo lake kuhakikisha kuwa kamwe
hawavishiwi roho za uoga kwa kuwa roho hizo za uoga kama zitakuwepo
ndani ya jimbo lake ni wazi kuwa wataendelea kuteseka na CCM

 

Maelezo Na: Gladness Mushi, FullShangwe

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO