Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hii ndio nyumba ya Waziri Maige anayodai kuinunua kwa USD 410,000

nyumba-maigeEzekiel Maige wa Maliasili na Utalii baada ya tuhuma, ameibuka na kukiri nyumba yake hii iko Mbezi Beach, Dar es Salaam, na ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).

Awali, habari zilizolifikia gazeti la Mwananchi zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate. Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hilo kwamba Waziri Maige amenunua nyumba moja kati ya nne zilizoko sokoni.

Picha na Maelezo: Mwananchi Habari, 26th April, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO