Shughuli ya kwanza ya Bunge la saba lililoanza kikao chake leo mjini Dodoma ilikuwa ni kwa wabunge wapya wawili kula Kiapo cha Utii.
Wabunge hao ni Mheshimiwa Cecilia Danieli Paresso (Viti Maalum CHADEMA) aliyeteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi Kufuatia kifo cha marehemu Regia Estalatus Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari, na Mheshimiwa Joshua Nassari (CHADEMA) aliyechaguliwa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki uliofanyika tarehe 1 Aprili, 2012 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo marehemu Jeremiah Solomon Sumari (CCM).
Spika wa Bunge, Mh Anna Makinda aliita majina yao Bungeni ili waweze kuapishwa kama ilivyokuwa imepengwa lakini hawakuwepo, hatua ambayo ilimlazimu Spika huyo kuachia majukumu Kamati ya Uongozi ili ipange siku nyingine kwa ajili shugghuli hiyo.
Aidha, baadae mchana Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Mh Zitto Kabwe alizungumza na wanandishi wa habari na kueleza kuwa chama chake kimeomba radhi kwa jambo hilo liliotokea na kwamba haikuwa matarajio yao.
Nae Naibu Spika, Mh Job Ndugai katika mkutano huo huo alitoa taarifa ya Kamati ya Uongozi kuwa wabunge hao wapya watapishwa Alhamis ya wiki hii kwa mujibu wa ratiba mpya.
Mh Ndugai alieleza pia kuwa muda wa kumalizi mkutano huu wa Bunge umesogezwa mbele kidogo kutoka Aprili 21, 2012 iliyopangwa awali hadi 24 Aprili, 2012.
0 maoni:
Post a Comment