Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwili wa Steven Kanumba kuzikwa Makaburi ya Kinondoni Kesho Jumanne

Ratiba ya awali ambayo imetolewa na Kamati Ya Mazishi ya Muigizaji Steven Kanumba inaonyesha kwamba shughuli za kuuaga mwili wake zitafanyikia katika viwanja vya Leaders jijini Dar-es-salaam kuanzia saa 4 asubuhi na baadae atazikwa katika makaburi ya Kinondoni ambayo hayapo mbali na viwanja hivyo.

Uhakika wa Ratiba hii unafuatia kuwasili kwa mama yake mzazi akitokea Bukoba na yeye kutoa baraka zake kwa mtoto wake kipenzi kupumzishwa hapa hapa jijini Dar-es-salaam.Haijafahamika kama Baba mzazi wa Kanumba anayeishi Shinyanga naye ameafiki wazo hilo au la.

m Mama mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa (katikati aliyeshika tama), akiwa amezungukwa na ndugu,jamaa na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sinza-Vatican.

Steven Kanumba, muigizaji ambaye bila shaka tunaweza kusema ndiye alikuwa maarufu zaidi miongoni mwa waigizaji wa filamu za kitanzania(Bongo Movies) alifariki majuzi alfajiri kuamkia Jumamosi katika mazingira ambayo bado yanatatanisha na bado polisi wanaendelea na uchunguzi ingawa taarifa ya uchunguzi wao wa awali, iliyotolewa na RPC wa Kinondoni,Charles Kenyela, inaonyesha kwamba huenda marehemu amefariki kutokana na matumizi mabaya (alcohol abuse) ya pombe kali aina ya Jack Daniels.

Taarifa hiyo inafuatia mahojiano kati ya Polisi na muigizaji mwingine Elizabeth Michael “Lulu” ambaye inaaminika ndiye alikuwa na Marehemu ambapo awali kabla mauti hayajamkuta palitokea kutoelewana baina yao.Kwa mujibu wa maelezo ya Lulu, Kanumba alikuwa ametumia kinywaji hicho kwa wingi ana wakati wakiendelea na malumbano, alianguka na kujigonga katika ukuta wa chumbani hapo.

Hata hivyo, taarifa ya kitabibu(Post Mortem) kuchunguza chanzo cha kifo chake  bado haijawekwa wazi na  inatarajiwa kufanyika hivi leo(Jumatatu) na ukimalizika basi ndipo taarifa rasmi itatolewa na hivyo kubariki rasmi kuendelea kwa shughuli za mazishi hapo kesho.

j5 Rais Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kwa wageni mashuhuri nyumbani kwa Merehemu, Sinza jana

j7 Rais Kikwete akizungumza na wafiwa

j3 Rais Kikwete akisalimiana na mgodo wa marehemu jana, wakati alipokwenga kuhani msiba wa Kanumba na kutoa rambirambi zake

Source: http://newspoststz.blogspot.com/

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO