Kwa mujibu wa taarifa ya Habari ya saa 2 usiku leo, kupitia Star Tv, inaelezwa kuwa Jeshi la Polisi nchini linakusudia kumkamata Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambae yuko kwenye ziara ya kichama katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema.
Sababu za kutaka kumkamata ni kutokana na kilichoelezwa kuwa ni kwa kutoa kauli za uchochezi katika mikutano ya hadhara Mwanza na Geita.
Taarifa zinamkariri Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akiongea na vyombo vya habari leo na kumtaka Katibu Mkuu huyo kujisalimisha mwenyewe baada ya kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mikutano yake ya Mwanza na Geita.
Kaimu kamanda anasema wameshindwa kumtia nguvuni kwasababu wanadai aliondoka Mwanza kinyemela juzi kuelekea Dar.
Polisi wanasema Dr Slaa alitoa vitisho kwa Serikali kwa kuipa siku 3 iwatibu wabunge wa CHADEMA walioshambuliwa Jijini Mwanza siku moja kbala ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba uliofanyika April mosi mwa huu, na pia kulipa Jeshi la Polisi siku 7 likamilishe uchunguzi kwa sakata hilo.
0 maoni:
Post a Comment