Katika ukurasa wake wa Facebook hii leo, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ambae pia ni Mbunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano, Mh Zitto Kabwe ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya rushwa ya wazi kabisa kwa wabuge ili kuchagua wagombea fulani kwa uwakishili wa nchi katika Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi uliokuwa uanatarajiwa kufanyika April 17,2012.
Tayari kuna ombi la CHADEMA liliotumwa juzi likimtaka Spika wa Bunge, Mh Anne Makinda kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi huo ili kuweka sawa taratibu fulani ambazo zimeonekeana kama zimekiukwa kwa mujibu wa Mkataba wa Shirikisho la Afrika Mashariki, jambo ambalo limeonekana kubana uhuru wa kidemokrasia kwa wananchi kupata uwakilishi unaowastahili.
Zitto ameonesha masikitiko yake kiasi cha kuamua kuibatiza Tanzania kama “The Land of The Corrupt” aka “FISADISTAN” kutokana na kukithiri kwake kwa vitendo vya rushwa.
Bandiko lake kupitia' akaunti yake ya ‘Facebook’ limesomeka hivi "Rushwa inavyotembezwa katika uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki inatia simanzi sana. Haingii akilini kwangu kabisa kwamba Mbunge anahongwa ili kuchagua Mgombea fulani. Nchi hii inanuka uvundo. Uvundo wa Ufisadi. Sasa ni sahihi nchi hii kubatizwa jina jipya FISADISTAN 'The Land of The Corrupt'"
0 maoni:
Post a Comment