Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mchungaji Uwinkindi Kuhamishiwa Rwanda kabla ya Aprili 19: ICTR

 

Mchungaji Jean Uwinkindi

Na Hirondelle, Arusha

Mtuhuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye yuko mikononi mwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR), Mchungaji Jean Uwinkindi atahamishiwa nchini Rwanda kabla ya Aprili 19, 2012.

Aprili 5, 2012, Rais wa ICTR, Jaji Vagn Joensen, aliamuru kwamba Uwinkindi ahamishiwe Rwanda ‘’katika kipindi cha siku 14 kutoka tarehe ya amri hiyo’’ na kumwelekeza Msajili ‘’kufanya taratibu zote zinazohitajika kwa ajili ya kutekeleza amri hiyo.’’
‘’Rais anamwelekeza Msajili kuanza mara moja majadiliano na Rwanda kujua nini cha muhimu kufanyika ili kutekeleza uhamisho wa Jean Uwinkindi,’’ inasomeka sehemu ya uamuzi huo.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Rais pia amemwelekeza Msajili wa mahakama hiyo kuwateua wanasheria wa ICTR kwa kushauriana na yeye ili kuwa ‘’wasimamizi wa muda’’ wa kesi hiyo pindi Uwinkindi atakapohamishiwa nchini Rwanda na hadi hapo Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) au chombo kingine kitakapoteuliwa rasmi kuwa msimamizi wa usikilizaji wa mwenendo wa kesi ya Uwindikindi.

Maelekezo hayo pia yanamtaka Msajili kuendeleza majadiliano tena na ACHPR kwa lengo la kuongeza kasi ya kukamilisha makubaliano husika ili kusimamia mwenendo wa kesi na kumwarifu Rais huyo haraka iwezekanavyo iwapo kutajitokeza ugumu wowote ili aone namna ya kusaidia au kufanya vinginevyo.

Juni 28, 2011, ICTR ilipitisha uamuzi wa kuhamishia kesi ya Uwinkindi nchini Rwanda na uamuzi huo kuthibitishwa na Mahakama ya Rufaa Desemba 16, 2011.

Kesi nyingine mbili pia zimeamriwa kupelekwa nchini Rwanda ambazo zinawahusu watuhumia wawili ambao bado wanasakwa na mahakama hiyo.Watuhumia hao ni pamoja na Fulgence Kayishema na Charles Sikubwabo.

Pia Aprili 12, 2012,  ICTR itasikiliza maombi mengine ya mwendesha mashitaka kutaka kesi ya mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo, Bernard Munyagishari, kwenda kusikilizwa nchini Rwanda.

Mchungaji Uwinkindi anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi.

Chanzo: John Badi (DAILY MITIKAS BLOG)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO