Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kutoka Bungeni: Joshua Nassari na Celcilia waapishwa rasmi leo, “Chenji” ya rada kutumika Elimu ya Msingi nchini

Shughuli ya kwanza ya Bunge la 10, Mkutano wa 7 Kikao cha 3, siku ya leo ilikuwa ni kuwaapishaa wabunge wapya wawili ambao hawakuweza kula Kiapo cha Utii juzi jumanne katika Kikao cha kwanza Bunge hili lilipoanza.

Wabunge hao ni Mheshimiwa Cecilia Danieli Paresso (Viti Maalum CHADEMA) aliyeteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi Kufuatia kifo cha marehemu Regia Estalatus Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari, na Mheshimiwa Joshua Nassari (CHADEMA) aliyechaguliwa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki uliofanyika tarehe 1 Aprili, 2012 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo marehemu Jeremiah Solomon Sumari (CCM).

Cecilia ndie alieanza kula kiapo na kufuatiwa na Nassari huku wote wakishangiliwa na baadhi ya wabunge waliohudhuria.

Baada ya kuongozwa kula kiapo cha utii, wabunge hao wapya walikabidhiwa nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Bunge kama vitendea kazi.

Katika tukio jingine Bungeni, Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda amesema fedha ambazo zilirudishwa kama ‘chenji’ kwenye ununuzi wa rada, ununuzi ambao ulizidi gharama halisi ziko Benki Kuu na zitawekwa kwenye akaunti maalumu ili kuweza kufuatilia matumizi yake.

Pinda amesema hayo wakati akijubu swali la Mbunge wa Iramba Mashariki, Mh Mwingulu Nchemba alietaka kujua swala la fedha hizo, katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni asubuhi ya leo.

Mh Pinda amesema fedha hizo, jumla ya Shilingi Bil 72.3 (Pound 29.5 Millioni) zimepatikana kupitia Benki Kuu ya Tanzania baada ya mazungumzao na kutiliana saini za makubaliano baina ya Serikali, DFID (Shirika la Misaada la Uingereza) pamoja na BAE System.

Waziri Mkuu amesema, sehemu kubwa ya fedha hizo, kwa mujibu wa makubaliano waliyosainiana tayari, zitaenda kusaidia sekata ya Elimu ya Msingi kwa mfumo wa “Capitation Grant” kupitia TAMISEMI ili kusaidia kutatua matatizo ya Shule za Msingi nchini hususani uhaba wa vitabu, na kiasi kidogo kitabaki Wizarani kwa ajili ya kuhudumia zoezi hilo.

Baadhi ya matatizo ya shule ya Msingi yatakayoenda kutatuliwa na fedha hizo, Pinada alitaja vitabu vya kiada na visivyo vya kiada, vitabu vya kufundishia.

Akifafanua zaidi namna fedha hizo zitakavyotumika, Waziri Mkuu amesema sehemu ndogo ya fedha hizo zitatumika kuondoa tatizo la uhaba wa madawati kwa Halmashauri 9 nchini.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi kufuatilia ili kuhakikisha vitabu vilivyokusudiwa vinapatikana kipindi fedha hizo zikianza kutawanywa kwa matumizi yake.

Akihitimisha majibu yake, Mh Pinda ameeleza kuwa hata ofisi ya CAG itahusishwa kufanya ukaguzi wa namna zitakavyotumika na kwamba kutakuwa na utaratibu maalumu wa kuzitoa fedha hizo toka kwenye akaunti maalumu itakayokuwa ikisimamiwa na BOT.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO