Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA kukata rufaa kupinga hukumu iliyomvua ubunge Godbless Lema

DSCN0026

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kinakusudia kukata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania dhidi ya hukumu ya Mhakama Kuu kanda ya Arusha iliyotolewa juzi Machi 5, 2012 na kuamua kumvua ubunge aliekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godbless Lema.

Akitangaza tamko hilo la chama, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, ambae pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe alisema chama chake kimetafakari na kuangalia misingi yote ya sheria kama chama makini, chama chenye dhamira ya kweli kukamata dola, na hivyo kuamua kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo badala ya kuingia kwenye uchaguzi mwingine kama ambavyo wananchi wengi wa Arusha na maeneo mengine walikuwa wakishinikiza.

Akihutubia maelfu ya watu waliojitokeza kwa wingi kwatika viwanja vya NMC mjini Arusha, Mbowe alisema CHADEMA inaamini uwepo wa Mahakama na inaheshimu uwepo wake nchini. Kwa swala la Lema kuvuliwa ubunge, Mbowe alisema bado wanaona zipo fursa nyingine za kuipata haki yao kisheria na endapo hazitaweza kuwasaidia ndipo watajua hatua nyingine ya kuchukua, ikiwemo kurudia uchaguzi.

“Mahakama haijamhukumu (Godbless) Lema, jaji ndie amemhukumu Lema” alisema Mbowe na kuwataka wananchi kutozilaumu Mhakama kwa ujumla wake kwasababu makosa hufanywa na watu.

DSCN9978 Mbowe alizitaja sababu tatu za chama chake kutoamua kuingia kwenye uchaguzi mwingine kwasasa na badla yake kuamua kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani, rufaa ambayo itawsilishwa Mhakamani jumanne ya wiki ijayo.

Akitaja sababu ya kwanza, Mh Mbowe alisema kukubali kuingia kwenye uchaguzi mwingine katika hatua ya sasa ni kukubali kuwa Mh Lema alikiuka taratibu za uchaguzi na hivyo ni wazi kuwa alishinda kwasababu alikiuka taratibu hizo, kitu ambacho alisema sio kweli.

Mh Mbowe alisema sababu ya pili ni ya kisera, kwamba CHADEMA kinapigania kuona matumizi sahihi ya rasilimali za taifa katika kutatua kero za wananchi kwa hiyo haitakuwa sahihi kukubali kuona fedha nyingi zikipotea kwenye uchaguzi uliotokana na maamuzi ya watu wachache. Alisema takribani sh bil 3 zinaweza kupotea kwenye uchaguzi huo, fedha ambazo ni kodi za wananchi ambao wanakabiliwa na shida nyingi.

“Hatutaki kupoteza fedha zenu.Serikali yetu ni ya kifisadi, ambayo viongozi wake watataka wapate fursa ya kula pesa zenu. CHADEMA tunataka matumizi sahihi ya fedha zenu, na sio zikarudie kwenye uchaguzi kwa maamuzi ya watu wachache” alisema Mbowe.

Sababu ya tatu kwa mujibu wa Mh Mbowe ni umuhimu wa kupeleka kile alichoita “injili” ya ukombozi katika maeneo mengine ya nchi na kwamba Mh Lema atakuwa na jukumu la kufanya shughuli hiyo kwa kipindi ambacho hatakuwa na majukumu ya Ubunge.

Aidha, Mh Mbowe alisema chama chake kina imani kubwa na Mahakama ya Rufaa nchini na kuiomba iangalie namna ya kuharakisha kushughulikia rufaa yao wanayotarajia kuiwasilisha jumanne ya wiki ijayo.

Mbowe alisema kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, rufani za kesi za uchaguzi huwa zinakuwa zimemalizika ndani ya kipindi cha miezi 12 ambapo jopo la majaji watatu huamua hatma ya shauri husika na kuamua ama kubatilisha hukumu ya awali (ya Mahakama Kuu) au kukubaliana nayo.

Tahadhari kwa Serikali ya CCM

Mbowe aliitaka serikali kuheshimu taratibu za kupata viongozi kwa njia za kidemokrasia na kueleza kuwa amani na utulivu wa nchi hauko mikononi wa Polisi kama wanavyotaka watu waamini, bali upo mikononi mwa watanzania wote.

Alitaadharisha kuwa endapo serikali itaendelea kutoheshimu maamuzi ya wananchi kujichagulia viongozi wao, ipo siku wataacha kupitia sanduku la kura na kuamua kuingia barabarani.

Katika tukio jingine, wananchama wanne wa CCM walikabidhi kadi zao za CCM kwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA na kutangaza rasmi kukihama chama chao na kuwa wananchama wapya wa CHADEMA.

DSCN9966

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO