Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Baada ya kuichachafya Serikali Bungeni, Wabunge wa CCM watishiwa maisha

BAADHI ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi, walioshiriki kusaini hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa nia ya kushinikiza kujiuzulu kwa mawaziri wanaotuhumiwa kufuja mabilioni ya fedha, wametishiwa maisha.

Habari za kuaminika zilizothibitishwa na mmoja wa wabunge hao, zimesema kuwa wabunge wawili kati ya wanne wa chama hicho wamelazimika kuukimbia mji wa Dodoma na kujificha kwa muda kusikojulikana.

Wabunge hao (majina yao tunayo) waliondoka mjini Dodoma mara baada ya kupewa taarifa na watu wao wa karibu kuwa walikuwa wakisakwa kwa vile baadhi ya wakubwa ndani ya CCM walikuwa wamechukizwa na kitendo hicho.

Read more on Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO