Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Spika Anne Makinda apinga zoezi la kukusanya saini za wabunge linaloratibiwa na Mh Zitto Kabwe ili kuwezesha kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda; Lissu ambana akubali

Spika  Anne Makinda SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda ameeleza kuwa zoezi la kukusanya saini za wabunge linaloratibiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh Zitto Kabwe, ni batili na linakiuka Kanuni za Bunge.

Zoezi hilo la ukusanyaji saini linafayika ili kufikisha idadi itakayoruhusu mbunge kupeleka hoja ya kulitaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ambapo kama kura hiyo itapigwa na wabunge wengi kuamua kutokuwa na imani nae, basi Rais atalazimika kuteua mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge (2007), inahitajika 20% ya wabunge waridhie kusudio la kupeleka hoja Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, ndipo mbunge mwenye hoja hiyo anaweza kuiwasilisha.

Akifafanua zaidi Bunge lilipokutana tean jioni, Spika Makinda alisema Kanuni za Bunge (2007) kifungu cha 133 (3)(a) na Katiba ya Nchi, kusudio la kutaka kumuondoa madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae likiwa katika taarifa ya maandishi, linapaswa kuwasilishwa kwa Spika wa Bunge siku 14 kabla.

Kwa mujibu wa Kanuni hiyo, ni wazi kuwa haitawezekana kusudio hilo kuwasilishwa kwa Spika na kufanyiwa kazi siku ya Jumatatu, siku ambayo Bunge litahitimisha vikao vyake kwa mkutano huu wa Bunge la 10.

Hata hivyo, Spika Makinda alisema kusudio hilo linaweza kufanyiwa kazi katika mkutano wa Bunge ujao, na kuwataka wahusika wahakikishe wanawalisha kusudia lao ndani ya muda ambao unakubalika kikanuni.

Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo.

Zoezi la kukusanya saini limekuwa na mafanikio makubwa kwa siku ya leo. Hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Mh Zitto Kabwe kwamba zaidi ya wabunge 50 wameweza kuweka saini zao hadi kufikia mchana wa leo kuridhia kusudio hilo wakiwemo baadhi ya wabunge wa CCM.

Miongoni mwa wabunge wa CCM waliotia sani fomu hizo maalumu ni pamoja na Mbunge wa Ludewa, Mh Filikunjombe ambae alisema saini aliyoweka sio yake binafsi, bali ni ya wananchi wa Ludewa waliomtumna na watanzania ka ujumla.

Mh Zitto alikuwa akisaidiwa na wabunge wenzake wawili wa CHADEMA, Mh Joshua Nassari, Mbunge mpya wa Arumeru Mashariki, pamoja na Mbunge wa Mbozi Magharibi, Mh David Silinde, ambao ni miongoni mwa wabunge vijana zaidi katika Bunge hilo.

Baadae Spika akubali kuwasilishwa kwa hoja ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu siku ya jumatatu, baada ya Mh. Tundu Lissu kuomba muongozo

Tindu-Lissu Muda mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini Dodoma, Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu ambae pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la kukusanya saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mh. Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa Kanuni na Sheria za Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Baada ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo, Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika, kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?

Mh. Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa Jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wananchi waliohojiwa kuhusiana na zoezi hilo wameeleza kufurahishwa kwao na jitihada za Mh Zitto katika kupigania rasilimali za taifa na uwajibikaji wa viongozi wa Serikali.

Wamesema hatua hiyo itarahisisha utekelezaji wa kuwajibisha viongozi walioshutumiwa kwa Wizara zao kuhusika na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.

Wakaeleza zaidi kuwa Waziri Mkuu alipaswa kuwa wa kwanza kuwawajibisha mawaziri hao na viongozi wengine, na kutolea mfano wa Halmashauri ya Kishapu ambayo imegundulika kutafuna zaidi ya Bil 6 na wahusika wanajulikana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

Source: StarTv Habari na Issa Michuzi, 20th April 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO