Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Arusha kupokea wageni 3,000 kwa mkutano wa Benki ya Afrika (AfDB)

WAKUU wa Nchi  za Afrika wasiopungua saba na magavana wa Benki Kuu wapatao 100, watakuwa miongoni mwa viongozi wa juu watakaohudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) utakaofanyika Mei  28 hadi Juni Mosi mwaka huu katika Jengo la Mikutano la Kimataifa la Arusha(AICC).

Mkurugezi Mkuu wa AICC, Elishilia Kaaya alisema  hayo alipozungumzia maandalizi yanayofanyika sasa kuhusu mkutano huo.
Alisema mkutano huo utakuwa wa aina yake kufanyika mjini hapa utakaodhuriwa na watu wapatao 3,000 kutoka sekta za mabenki na wafanyabishara wakubwa mbali na maofisa wengine kutoka nje na ndani ya nchi.

Alisema kutokana na umuhimu wa mkutano huo, uongozi wa AICC umelazimika kuhama ofisi zake vyumba vipatavyo 110 ili kupisha maofisa wa AfDB kuanza maandalizi ya mkutano huo utakaoleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika Mji wa Arusha.

“Tunaiomba Serikali kufanya tathmini kwa kutumia wataalamu wake wa takwimu ,kuona ni kwa kiasi gani uchumi wa mkoa huu utabadilika kutokana na ujio wa mkutano huu ili kuwawezesha  wananchi kuona umuhimu wa mikutano kama hii kufanyika hapa,”alisema Kaaya.

Kaaya alisema kama Taasisi ya Serikali imetenga  Sh1.2 bilioni kwa ajili ya maandalizi ikiwa ni pamoja na  kuongeza vifaa vya taafsiri, mahema makubwa  yatakayotumika kwenye maonyesho ya mabenki na shughuli mbalimbali katika mkutano huo.
Mara ya mwisho mkutano  kama huo ulifanyika mjini Lisbonne nchini Ureno mwaka 2010.

Wakati huohuo, Kaaya alisema mradi wa ujenzi wa maduka ya kisasa eneo la Soweto mjini Arusha utakaoshirikisha taasisi hiyo na Mfuko wa Pensheni wa wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF) utaanza hivi karibuni baada ya waliokuwa wapangaji kuhama bila usumbufu.

“Napenda kuwapongeza waliokuwa wapangaji wetu eneo la Soweto kwa kuona umuhimu wa kuhama bila usumbufu,nataka wasione kama eneo hilo haliendelezwi baada ya wiki moja nyumba zote zitakuwa zimebomolewa kupisha ujenzi huo,”alisema Kaaya.

Published by Mwananchi, 25th April, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO