Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Tawi jipya la benki ya BancABC nchini lazinduliwa na Makamu wa Rais Jijini Arusha leo

AR 1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya ACB ya jijini Arusha, Dkt. Jonas Kipokola, wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika Benki hiyo mpya wakati Makamu alipoizindua rasmi leo Aprili 16, 2012

AR4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya ACB muda mfupi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Benki hiyo mpya wakati Makamu alipofika jijini humo kuizindua rasmi leo Aprili 16, 2012 (Picha ya kwanza na ya pili na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais)

DSCN0019 Tawi hili jipya la benki ya BancABC kama linavyoonekana pichani lililoko Mtaa wa Swahili, Jijini Arusha

DSCN0022 Wateja wa mwanzoni wakipata maelekezo toka kwa watumishi wa benki kuhusiana na huduma za benki hiyo. Gharama za kufungua akaunti katika benki hii kama kianzio ni sh3,000 tu.

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na huduma za benki hii unaweza kutembelea website ya BancABC

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO