Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Vijana wanne waendesha bodaboda wapatikana wamenyongwa hadi kufa Mjini Arusha

DSCN0002 Miili ya watu wanne iliyopatika mapema alfajiri ya April 21, 2012katika maeneo tofauti ya Arusha, baada ya kunyongwa na watu wasiojulikana hadi kufa.

1  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti hapa. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru

Waliouawa kuwa ni dereva wa bodaboda, Laizer Nalaba (22) mkazi wa Mbauda, Jumbe Saitoti mkazi wa Sokon 1 , Elias Loting’idaki na Richard Maombi, maarufu kama ‘Boshuu’, ambao ni wakazi wa Sombetini.

Maiti moja ilipatikana eneo la Holy Ghost, Kata ya Akheri ikiwa pembeni mwa barabara wakati maiti mbili zilipatikana katika Kijiji cha Mlangarini chini ya Mto Nduruma na maiti nyingine ilipatikana katika Kijiji cha Nambala, Kata ya Kikwe.

Tanzania Daima (22April, 2012) linaripoti zaidi kwa uthibitisho wa Jeshi la Polisi

WAKAZI wanne wa Jiji la Arusha wameuawa kwa kunyongwa shingo kwa kamba na minyororo kisha maiti zao kutupwa katika maeneo mbalimbali kwenye Wilaya ya Arumeru.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye, alithibitisha kuwapo kwa matukio hayo ambapo alisema kuwa walipata taarifa za kuwapo maiti za wanaume hao kutoka kwa wananchi jana majira ya saa 12 asubuhi.

Aliwataja waliouawa kuwa ni dereva wa bodaboda, Laizer Nalaba (22) mkazi wa Mbauda, Jumbe Saitoti mkazi wa Sokon 1 , Elias Loting’idaki na Richard Maombi, maarufu kama ‘Boshuu’, ambao ni wakazi wa Sombetini.

Alisema kuwa maiti moja ilipatikana eneo la Holy Ghost, Kata ya Akheri ikiwa pembeni mwa barabara wakati maiti mbili zilipatikana katika Kijiji cha Mlangarini chini ya Mto Nduruma na maiti nyingine ilipatikana katika Kijiji cha Nambala, Kata ya Kikwe.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba watu hao waliuawa kwa kunyongwa kwa kamba shingoni na kisha kutupwa katika maeneo hayo,” alisema kamanda huyo wa polisi mkoani hapa.

Alisema kuwa maiti hizo zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru wakati polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji na wahusika wake ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

Miili ya watu hao kabla ya kutambuliwa iliwekwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ili waweze kutambuliwa na ndugu zao ambapo mmoja alikuwa na kamba shingoni na mwingine akiwa amefungwa mikono yake pamoja kwa mnyororo na mwingine alikuwa na jeraha kichwani, linalodhaniwa kutokana na kupigwa na kitu kizito.

Akieleza namna maiti hizo zilivyogunduliwa, Andengenye alisema kuwa wananchi wa maeneo ilipotupwa miili hiyo walipiga simu kwenye kituo cha polisi wilayani Arumeru majira ya saa 12 na saa moja asubuhi wakiwataarifu kuhusu matukio hayo.

Andengenye alisema kuwa inawezekana kabisa kuwa watu hao waliuawa sehemu tofauti kisha miili yao ikabebwa na kwenda kutupwa maeneo hayo, ambapo tofauti kati ya eneo lilipotupwa maiti moja na nyingine ni wastani wa kilometa mbili, ambapo kwenye baadhi ya maeneo zilionekana alama za matairi yanayodhaniwa kuwa ni ya gari lililotumika kubeba maiti hizo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa alielezea kusikitishwa na tukio hilo ambapo aliwasihi wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa polisi ili kufanikisha kubainika kwa chanzo cha mauaji hayo ya kinyama.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO