Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Alert: Zitto anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuelezea kusudio la kukabidhi Hoja ya ‘vote of no condidence’ kwa Spika kesho Jumatatu

Katika bandiko lake kwenye Facebook mchana huu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Mh Zitto Zubeir Kabwe amesema anakusudia kuzungumza na Waandishi wa Habari majira ya saa 9 alasiri katika viwanja vya Bunge, Dodoma.

Agenda kuu katika mkutano wake huo ni

1)Kuutaarifu umma kwamba sahihi 70 zimekwsihapatikana

2)Kuutarifu umma kwamba Spika (Anne Makinda) atakabidhiwa HOJA (ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu) kesho Jumatatu

3) Kutoa ufafanuzi kuhusu sharti la siku 14 kabla ya siku ya hoja.

Pinda kuwaumbua mawaziri kesho

Wakati huo huo Gazeti la Nipashe toleo la leo Aprili 22, 2012 linaripoti kuwa Waziri Mkuu Pinda amesema ataweka mambo hadharani kesho Jumatatu kuhusu hatima ya mawaziri wanaotuhumiwa, ikiwa ni pamoja na kama watamkabidhi barua za kujiuzulu.

Shinikizo la kuwataka mawaziri hao kujiuzulu, lilikuwa kubwa kuanzia kikao cha Bunge kilichoketi Alhamisi, ambapo wabunge wa CCM na upinzani waliungana kuwataka mawaziri hao kujiuzulu.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, Pinda alisema hadi sasa hajapokea barua ya kujizulu kutoka kwa Waziri yoyote.

Alipobanwa azungumzie habari zilizochapishwa kwenye baadhi ya magazeti kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri nane, Pinda alisema hajasoma magazeti hivyo hawezi kuzungumza chochote.

“Sijapata barua yoyote hadi sasa ila kama wapo watakaoleta nitapokea, ila mambo yote yatajulikana Jumatatu, siwezi kuyazungumza kwa sasa,” alisema Pinda.

Juzi usiku, wabunge wa CCM walifanya kikao cha dharura na miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya kikao hicho, ni mawaziri nane kutakiwa kujiuzulu wenyewe.

Mawaziri ambao ilisemekana kuwa walishinikizwa na wabunge wajiuzulu kwani wamekuwa mzigo kwa serikali ni pamoja na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika.

Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe.

Jana kuna habari zilizoenea mjini hapa ambazo hazijathibitishwa kuwa baadhi ya mawaziri wameshaanza kuandika barua za kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO