Ndege ya shirika la ATCL imeanguka mkoani Kigoma baada ya kushindwa kuruka wakati ikianza safari yake kuelekea Tabora na Dar es Salaam. Inaelezwa kuwa ndege hiyo imeharibika vibaya, na taarifa za uhakika zinasema kwamba hakuna abiria yeyote aliyeumia sana. Jumla ya abiria 41 wamenusurika kifo katika ajali hiyo na utaratibu wa kuwasafirisha abiria na majeruhi unafanywa jijini Dar es Salaam.
Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC), aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora, ikiwa imeanguka jana baada ya kuteleza kutokana na tope jingi kuwepo kwenye njia ya kurukia ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Abiria 35 na wafanyakazi wanne walinusurika kwenye ajali hiyo
Hali ya ndege inavyoonekana upande wa kushoto
Wananchi wakiangalia ajali ya ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC), aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora, ikiwa imeanguka jana baada ya kuteleza kutokana na tope jingi kuwepo kwenye njia ya kurukia ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Abiria 35 na wafanyakazi wanne walinusurika kwenye ajali hiyo
Hali ilivyokuwa inaonekana ndani ya ndege baada ya ajali kutokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Source: Mjengwa BLOG
0 maoni:
Post a Comment