Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wananchi Arumeru wavamia shamba la mwekezaji na kujigawia

Published by FULL SHANGWE, yesterday 22th April 2012

Wananchi wakazi wa Machumba kata ya Nkwandua wilayani Arumeru leo wamevamia shamba la mwekezaji linalofahamika kama Mashumba estate na kujigawia ardhi kwa madai kuwa wanafanywa watumwa kwenye nchi yao huku wakuja wakijitwalia maeneo na kufaidi rasilimali za nchi hii.

Wakazi hao wamavamia mashamba hayo yenye ukubwa wa hekari 400 saa 9 usiku wa kuamikia leo na kujigawia ardhi hiyo wakidai kuwa wanacheweshwa kupata ridhiki zao licha kuwa serekali ikwisha waambia kuwa wafanyesubra ilikulitatua tatizo la ardhi na mwekezaji huyo aliekimbia usiku wa leo.

Makundi ya vijana na kinamama walikuwa wakigawana ardhi ya shamba hilo huku wakisema sasa ndiyo mwisho wamafisadi kwani tumechoka kugandamizwa na kuwa watumwa katika nchi yetu ardhi yetu ya muhindi.

Walidai kuwa mzee Kirilo alikwenda UN kudai haki ya weusi kumiliki mashamba (Ardhi) lakini mashamba makubwa  yanamilikiwa na wenye hela wakati maskini tunaendela kutizama katika nchi yetu sasa tunasema basi kama kufia hapa alisema alfred Akyoo

Akyo alisema kuwa njia yakwenda vijiji vya kusini hadi chekereni lazima uzunguke shangarai na ukienda makusaro lazima uende Tengeru haya mashamba yamezuia njia zote na serekali haina la kusema njia nyepesi ni lazima upite katikati ya mashamba hayo

"Leo usiku vijana wa singi'si woanaenda kuvamia mashamba ya Sadc na baadae mashamba ya Gomba ESTATE katika muendelezo huo wa kudai haki zetu na kwa hili watatuulia hapa  hakuna kulala hadi kieleweke" alisema akyo.

Hataivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa arusha bado zinaendelea juu ya sakata hilo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO