Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM Yazidi Kumeguka Arusha, Diwani wa Kata Sombetini Nae Atangaza Kujiengua CCM

Diwani wa Kata ya Sombetini ya Jijini Arusha, Mh Alphonce Mawazo (CCM) ametangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoani Arusha, Ndg Samson Mwigamba, zinaeleza kuwa Mawazo ametangaza uamuzi wake huo leo asubuhi Mjini Dodoma.

Baadae alifanya mahojiano na Redio 5 ya Arusha na kueleza kuwa meamua kuachana na CCM kwasababu chama hicho kimeshapoteza muelekeo.

Amedai kuwa wananchi wake wanazo tarifa za uamuzi wake huo.

Hatua ya Diwani Mawazo kujiondoa CCM inakuja zikiwa zimepita siku mbili tu tangu aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, James Ole Millya kutangaza kujitoa CCM na Kujiunga na CHADEMA.

Katika hatua nyingine, kuna taarifa ambazo wahusika hawajapatikana kuthibitisha, zikieleza kuwa baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Themi akiwemo Bi Violet Mfuko ambae Mwenyekiti wa chama hicho katika Kata hiyo iliyo ndani ya Mji wa Arusha, nae ametangaza kuihama CCM na kujiunga na CHADEMA mchana wa leo.

Viongozi wengine waliojiengua CCM kwa mujibu wa taarifa hizo za ni Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM Arusha, Ndg Ally Banaga pamoja na Johna Nyiti ambae alikuwa Katibu wa Hamasa UVCCM Arumeru.

Pamoja na hayo, kulikuwa pia na taarifa za kujiengua kwa Katibu Mwenezi wa UVCCM Wilaya ya Longido jana, Ndg Yohana Laizer, ambazo tayari zimethibitishwa kuwa ni kweli nae amejiengua kutoka CCM.

Halikadhalika kuna taarifa ambazo bado hazijawa dhahiri kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha nae yuko mbioni kukihama chama chake.

Mpaka sasa ni jumla ya viongozi 5 wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi wameshatangaza kujiengua kutoka katika chama hicho kufuatana na taarifa zilizopatikana hadi sasa, sambamba na huyo Diwani wa Kata ya Sombetini, Alfonce Mawazo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO