Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mtei azungumzia Tume iliyoundwa ya Mbadiliko ya Katiba; Zitto ampinga

Yafuatayo ni maoni ya muasisi wa CHADEMA ambae pia aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu nchini, Mzee Edwini Mtei kama yalivyowekwa kama ‘thread’ katika mtandao wa Jamii Forum kama bandiko lake la jana kuelezea anachokiona kuhusiana na Tume ya Mabadikilo ya Katiba iliyoundwa mwanzoni mwa mwezi huu na Rais Kikwete.

Mtei na Tume ya KatibaBandiko halisi kwa hisani ya Mtanado wa KULIKONI UGHIBUNI 

“Licha ya kwamba J.K. kajitahidi kuwa na vigogo kweli kweli, na Katiba ya sasa imezingatiwa ktk kuandaa m'badala wake, muundo wa hii Tume umedhihirisha kwamba demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania wa leo. Kama tunanuia kwa dhati kuwa na Demokrasis ya kweli, itabidi Watanzania wanaoamini kwamba hilo ni muhimu, waendelee na juhudi za kuandaa hata Mabadiliko kwa Katiba Mpya ijayo.

Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.

Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.

Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.”

TAYARI zimeibuka tafsiri tofauti kuhusiana na maoni yake hayo. Mionzoni mwa waliotofautiana nae ni pamoja an Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Mh Zitto Kabwe ambae ameandika katika tweet mojawapo kutoka kwenye ukurasa wake ya “Tweeter” akisema “Yeyote anayeangalia #TumeyaKatiba kwa misingi ya #Dini za wajumbe amefilisika kimawazo, ni kirusi dhidi ya Utanzania wetu. Azomewe" kama inavyoonekana hapa chini…

zitto

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO