Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nape adai James Ole Millya alikuwa mzigo kwa CCM, ampongeza kujiondoa kwenye chama

DSCN0028

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Kamati Kuu ya CCM (NEC-CCM), Ndg. Nape Nnauye amezungumzia uamuzi wa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya kutangaza kujiengua CCM mapema leo asubuhi, na kusema kuwa uamuzi wake huo ni wa kukisaidia chama chake, CCM.

Maneno hayo ameyaandika katika bandiko lake leo mchana huu, majira ya saa nane kupitia ukurasa wake wa Facebook kueleza mtazamo wake na namna alivyopokea taarifa hizo za kujiengua kwa kiongozi wa vijana ngazi ya Mkoa.

Nape ameandika hivi (kama picha inavyoonesha hapo juu) “Nampongeza Millya kwa kuamua kukisaidia Chama Changu, kwani alishakuwa mzigo mkubwa kwa CCM. Itakumbukwa alikuwa afukuzwe kwenye chama kutokana na mambo alokuwa akifanya. Akapewa KARIPIO ili apate muda wa kurekebisha tabia yake! Kaondoka akiwa chini ya karipio. Kajivua gamba,tunampongeza kwa kuitikia wito wa kujivua gamba. Kila lakheri aendako ni kijana bado anayo mengi ya kujifunza!”

Katika sehemu ya madajiliano na marafiki zake kwenye ‘post’ yake hiyo, kuna rafiki mmoja (Neema Lema) alimuhoji Nape Nnauye “Kwanini hamkusema tokea mwanzo leo kajichia ndo mnachonga midomo wakatimlijua fika kuwa siyo mtu mwema?”

Majibu ya Nape kwa swali hilo yalikuwa hivi “Lema@ uliza kwanini hatukurudisha jina lake kwenye East Africa?”

Kwa kitendo cha Nape kumhusisha James Millya na kushindwa kwake kupita katika mchujo wa uteuzi kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (kama alivyojibu hapo juu) kinashabihiana na taarifa ambazo hazijathibitishwa na Millya mwenyewe, zikieleza kwamba moja ya sababu ya Milly kujiengua CCM ni pamoja na kuhujumiwa katika haki yake kuwania nafasi hiyo ya uwakilishi na baadhai ya watu ndani ya chama chake.

nape's Katuni hii pia inapatikana katika ukurasa wa Mh Nape kupitia matandao wa Facebook, aliibandika jana

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO