MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa imekamilika na vitaanza kutolewa mapema mwezi ujao.
Imesema kuwa uzinduzi wa kutoa vitambulisho hivyo ulikuwa ufanyike jana katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini ilishindikana kutokana na shughuli nyingi na ukubwa wa tukio hilo.
Ofisa Habari wa NIDA, Rose Mdami alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Rais Jakaya Kikwete ambapo wiki ijayo watazungumza na waandishi wa habari na kuelezea utaratibu mzima utakavyokuwa.
Wakati huo huo Ndg Dickson E. Maimu, Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) anautangazia uma kwamba…
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inapenda kuwafahamisha Wananchi wote kuwa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu limeanza kwa Wafanyakazi wa Umma kwa Dar es salaam na Zanzibar
Aidha zoezi hili litafanyika kwa awamu katika kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha kwamba kila mtu amesajiliwa na kupewa Kitambulisho chake
Zoezi hili halitahitaji malipo ya aina yeyote, fomu za Usajili na Utambuzi zitatolewa bure.
Tunapenda kuwatahadharisha Wananchi kutokubali kununua fomu mtaani au kulipia gharama zozote za usajili ikiwemo kuhakiki makazi anayoishi mwombaji katika zoezi linaloendelea.
Tafadhali toa ushirikiano iwapo utabaini fomu kuuzwa au kutozwa gharama zozote kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwa simu namba 0767 410251/2, 0687 450201, 0658 100200/300.
0 maoni:
Post a Comment