Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SABODO AFURAHISHWA NA USHINDI WA CHADEMA ARUMERU MASHARIKI, AIMWAGIA SH.MIL 100

 

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo (kushoto) akitia saini kwenye hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 alizotoa msaada kwa Chadema, baada ya kufurahishwa na ushindi wa chama hicho katika Jimbo la Arumeru Mashariki Jumapili. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Antony Komu. Hafla hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Sabodo Upanga, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa (kulia),
akimshukuru mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo baada ya chama hicho kupatiwa msaada wa sh. mil. 100, kwa kufurahishwa na ushindi wa Chadema katika uchaguzi uliofanyika  Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha Jumapili. Hafla hiyo ilifanyika, Dar es Salaam

PICHA &MAELEZO: KAMANDA WA MATUKIO, Richard Mwaikenda

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO