Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UVCCM Arusha wapingana katika shutuma dhidi ya James Ole Millya aliehamia CHADEMA

GAMBOMjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) taifa anaewakilisha Mkoa wa Arusha, Ndg Mrisho Gambo amemshushia lundo la shutuma aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya ambae alijitoa CCM na kujiunga na CHADEMA mapema wiki hii, na kudai kuwa hakuwahi kufanya jambo lolote la maana kwa chama chake hicho cha awali.

Bw Gambo amedai kuwa Millya hakuwa mwaminifu, ni tapeli na kwamba wao kama UVCCM wanafurahia kuondoka kwake.

Akadai pia kuwa James Millya ameondoka bila kukabidhi ofisi sambamba na hesabu zinazofikia thamani ya sh mil 600.

Akitolea mfano wa shutuma hizo, Mrisho Gambo (pichani) amesema kuwa James Ole Millya aliwahi kuhusika na upotevu wa sh mil 2 zilizotolewa kwa ajili ya ‘saccos’ ya UVCCM Arusha.

Amedai fedha hizo zilitolewa mwaka 2008 na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini wakati huo, Ndg Felix Mrema kwenye mkutano wa Baraza la Vijana wa CCM lililofanyika Mjini Karatu.

Katika hali ya kubatilisha kile alichoeleza Gambo, mjumbe mwingine wa Baraza hilo ambae aliwahi kuwa Mwenyekiti wa umoja huo kipindi cha nyuma, Ndg Ally Bananga alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha vikali kuhusihwa kwa James Ole Millya na ubadhirifu huo wa sh mil 2 zilizolenga kusaidia ‘saccos’ ya UVCCM.

Bananga alikuwa pamoja na mjumbe mwingine toka Arumeru, Boniface Mungaya wamesema shutuma hizo za Mrisho Gambo sio za kweli na kwamba maswala ya fedha za umoja huo husimamiwa na taratibu maalumu za ofisi, lakini pia wakakiri kuwa ni kweli kuondoka kwa Millya ni pigo kwa umoja huo.

Akifafanua zaidi, Ally Bananga ameeleza kuwa fedha zote za saccos zilikuwa zikisimamiwa na Kamati Maalumu.

Mrisho Gambo alishiriki na kuangushwa na kina Adam Kimbisa, Charles Makongoro, na Bernad Murunya ambao waliibuka washindi kwenye kinyang’anyiro cha kuwapata wabunge wawakilishi wa Tanzania Bara katika Bunge la Afrika Mashariki, katika uchaguzi uliofanyika April 17, 2012.

Ole Millya nae alipohojiwa kuhusiana na shutuma hizo alikanusha kuhusika nazo na kudai kuwa hiyo ni dalili ya kuweweseka baada ya kuondoka kwake.

Akadai kuwa atahakikisha anawajulisha watanzania maovu yote ya CCM

CHADEMA wazidi kuvuna madiwani wa CCM

Wakati hayo yakiendelea, taarifa kutoka Mkoani Mwanza zinaeleza kuwa Diwani wa Kata ya Lugata, Wilayani Sengerema, Mh Adrian Tizeba amekihama chama chake cha CCM na kujiunga rasmi na CHADEMA. Taarifa hizo zinaongeza kuwa kesho inatarajiwa madiwani wanne zaidi kutoka Jimbo la Sengerema na Wenyeviti wa vitongoji 22 watajiunga na CHADEMA.

Kutoka Arusha nako, jumla ya wanachama 2400 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Ngorongoro wamejivua uanachama wa CCM na kujiunga na CHADEMA.

Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na Katibu wa CHADEMA Mkoani Arusha, Ndg Amani Golugwa zinaeleza kuwa miongoni mwa wanachama hao ni pamoja na Wenyeviti 5 wa Vijiji vilivyoko Kata ya Ngorongoro.

Wananchi hao walioikimbia CCM wanaongozwa na Bw Saitabao Teretu kutoka Esluway-Endulen akiwa na wanachama 478, mwingine ni Bw Kone Teima kutoka Ngiani ambae yuko na watu 590.

Viongozi wengine ni Bw Marko Mbeme wa kijiji cha Ngiyapase ambae yuko na wanachama takribani 600, BwSaruni Mengarana waEmbarway mwenye watu 224 pamoja na Bw Robert Edward wa Madukani ambae yuko na wafuasi 520.

Chanzo: StarTv Habari, ITV na Daily News, 20 April, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO