Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ANDIKO LA BEN SAANANE KUFAFANUA UPOTOSHAJI WA TAARIFA ZA KUFUKUZWA KWA JULIANA SHONZA BAVICHA

Japo sikutaka kujibu hoja ya Shonza; maana si jambo zuri sana kujibu tuhuma ambazo zimetolewa na watu nje ya CHADEMA. Watu ambao hadi muda huu si wanachama wa CHADEMA, lakini kwa kuwa lengo la maadui wa CHADEMA (CCM na vibaraka wake) ni kueneza uongo dhidi ya CHADEMA, Viongozi na wanachama wake basi hatuna budi kujibu uongo huo kwa kusema ukweli.
Naomba nijibu machache yanayonihusu ili kuweka kumbukumbu sawa kwa kuwa uongo unapoandikwa na ukabaki hivyo bila kutolewa ufafanuzi unaweza kusababisha watu wakanukuu kitu ambacho siyo sahihi.
MOSI:
Sijawahi kumchafua kiongozi yeyote na sijawahi kuomba msamaha mahali popote kuhusiana na kumchafua kiongozi yeyote. Nilishawahi kulisema hapa, lengo la propaganda hii ni kutaka kuyumbisha mawazo ya watu na kuwafanya waamini kwamba yote niliyosema huku yalikuwa na lengo la kumchafua mtu. Nasizitiza kwamba kila nilichoandika ni sahihi na kamwe sitaomba radhi kwa lengo la kumridhisha yeyote. Nitausimamia ukweli tu na hakuna maridhiano nje ya ukweli.
Niliomba msamaha kuhusu kushirikiana kwangu na kundi la MASALIA/PM-7 na pia kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yangu kwa njia ya mtandao badala ya kufuata taratibu za vikao.
PILI:
Hoja kwamba nilisamehewa si kweli. Nilipewa adhabu ya Onyo kali na kuwekwa chini ya Uangalizi kwa kipindi cha miezi 12 kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa vijana kwenye vyombo vya habari na pia mimi binafsi kupokea barua tarehe 11/01/2013.Naelewa taratibu za vikao na naiheshimu katiba ya CHADEMA,kanuni,itifaki na maadili ya CHADEMA.
Tarehe 12/01/2013 niliandika barua ya kukata rufaa na nikatoa sababu ni kwanini siridhiki na hukumu iliyotolewa dhidi yangu.
Nilitekeleza wajibu huu kwa kuzingatia Kanuni, Itifaki na katiba ya chama chetu katika sura ya 5 Ibara ya 2 kifungu cha 4 kama inavyoelekeza juu ya haki za Mwanachama naomba kunukuu ‘’5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu kichama’’
Huu ndiyo utaratibu uliowekwa na unaoongozwa ma katiba ya CHADEMA kama hujaridhika na uamuzi uliotolewa kwenye ngazi za chini kuna ngazi za rufaa.kuna kamati kuu, kuna Baraza kuu n.k
TATU:
Hoja ya kuangalia watu wametoka wapi (ukanda) haina mantiki kikanuni, kikatiba na haiwezi kuwa hoja yenye uzito kwa Chama au Taifa linalojali misingi ya haki na maadili. Ni lazima nihukumiwe kulingana na Tabia yangu. Si sahihi kusema nimehukumiwa au kusamehewa kwa sababu ni Mchagga au Mkristu. Vigezo hivi vinatumika na maadui wa CHADEMA tu. Leo tumeshuhudia kigezo kingine cha jinsia kikitumika katika hoja ya Shonza ili kupata huruma (sympathy).
Katika walioenguliwa BAVICHA na mimi ni mmojawapo, hilo halitajwi kwa makusudi maalumu.
Katika adhabu niliyopewa, inalingana na adhabu ya Kasambala na Gwakisa kutoka Mbeya (Kama vigezo vya ulikotoka ni vya Msingi) tujiulize mbona nimehukumiwa na hawa wanapotosha wanasema nimesamehewa? Wote tuna fursa ya kukata Rufaa kwa mujibu wa kanuni niliyotaja hapo juu!
Sikuchagua kuzaliwa kabila fulani. I view it as wrong and unethical to discriminate against someone based on who they are – that is, based on what ethnic background or skin color they are, or any other trait that is beyond one’s choice.
NNE:
Sijawahi kutumwa na kiongozi yeyote kuanzisha PM-7 tofauti na viongozi na wanachama walioshiriki kikamilifu ambao niliwataja katika tamko langu lililopita
TANO:
Uchaguzi wa BAVICHA tuligombea tukiwa tunajua kuhusu suala la kadi za BAVICHA na hakuna hata mmoja aliyewahi kuhoji hili. Tumpuuze mtu yeyote anayetaka kubadili kanuni na sheria hasa pale anapoona kuna maslahi yake tu. Tukiruhusu viongozi wa aina hii tutakuwa tunaandaa taifa la hovyo.
Mtu huyo huyo anayejenga hoja ya kitoto kuwa hakuna unachama wa BAVICHA na hivyo kutoa taswira ya kuwa BAVICHA haipo kihalali ndani ya muda mfupi tu anajitangaza kama Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA... Inashangaza!
SITA:
Tuendelee kusonga mbele na tuwapuuze hawa wanaotumiwa kufifisha nguvu ya Mabadiliko kwa kutunga uongo, uzushi na ghiliba ili malengo yatimie. Hawa tuwapimie kipimo kile kile kinachotumika dhidi ya CCM na maadui wa CHADEMA. Waache waendelee na matamko mfu yanayofadhiliwa na maadui zetu akiwemo yule aliyekuwa anatumia nguvu nyingi kudai posho ya wabunge iongezwe hadi kufikia laki 5 kwa siku (na kuibatiza jina-UJIRA WA MWIHA) ili aweze kufadhili uasi dhidi ya CHADEMA.
Naanza mchakato wa kisheria dhidi ya wale waliotoa madai na tuhuma za kuuana kwa kuwa ile ni jinai, zaidi ya hatua za kisiasa ni lazima nichukue hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa vijana wanaotumika vibaya ndan ya mfumo wetu wa siasa.
Mengine nitaachia mamalaka husika na taratibu za Vikao kwa mujibu wa Katiba, Maadili na Itifaki ya Chama.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO