Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAHAKAMA KUU YAMWACHIA LULU KWA DHAMANA, YATOA MASHARTI MATANO

Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imemuachia huru msanii wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael maarufu Lulu baada ya kumpa masharti matano ambayo anapaswa kuyatekeleza.

Moja vigezo vilivyoisukuma mahakama hiyo kumuachia uhuru ni kwa sababu shtaka lake linadhaminika, sharti la pili Lulu anatakiwa kusalimisha kwa msajili wa mahakama hiyo hati zake za kusafiria kutoka nje ya Jiji La Dar es Salaam bila idhini ya mahakama, na sharti la tatu, kuripoti kwa msajili wa mahakama kila mwezi.

Katika sharti la nne Lulu anatakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikali, na sharti la tano, wadhamini hao anapaswa kusaini bondi ya Sh20 milioni.

Awali jopo la mawakili wa Lulu ambalo linaongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Petere Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wiki iliyopita waliwasilisha  maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo.

Maombi hayo, yalikuwa yamepangwa kusikilizwa wiki iliyopita na Jaji Zainabu Mruke, lakini yalipelekwa mbele mpaka yaani LEO Jumatatu siku ambayo amepewa dhamana.

Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii maarufu wa fani hiyo nchini, Steven Kanumba.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia kinyume cha kifungu cha 196.

Katika hatua nyingine za kisheria baada ya upelelezi kukamilika, Desemba 21, mwaka jana, Mkurugenzi wa Mashtka  (DPP) alimbadilishia Lulu Mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia.

Chanzo: HabariMaasai.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO