Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Makala ya BBC: Ethiopia tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika

Timu ya Taifa ya Ethiopia

Timu ya taifa ya Ethiopia

Ethiopia iliandikisha matokeo mema wakati wa michuano ya kufuzu kwa fainali ya mataifa ya Afrika, kwa kufungwa magoli matano pekee.

Iliifungwa na Sudan magoli matano mjini Khartoum, na kufuzu kwa fainali hizo zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini, kuambatana na sheria ya goli la ugeneini, baada ya kufungwa magoli mawili kwa bili mjini Adis Ababa, Ethiopia.

Mashabiki wa timu hiyo ya taifa ya Ethiopia, maarufu kwama Walias Antelopes, walishangilia usiku kucha, katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo kusherehekea kufuzu kwa timu hiyo.

Antelopes kucheza na Chipolopolo

Ethiopia imeratibiwa kucheza mechi yake ya ufunguzi na mabingwa watetezi wa kombe hilo la Mataifa ya Afrika, Zambia tarehe 21 mwezi huu katika uwanja wa Mbombela mjini Nelsruit Afrika Kusini.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Ethiopia kushiriki katika nafali hizo za Afrika kwa zaidi ya miaka thelathini iliyopita.

Ethiopia, imejumuishwa katika kundi moja na Zambia, Nigeria na Burkina Faso, kundi C.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ethiopia

Miaka thelathini na moja iliyopita katika fainali hizo Ethiopia pia ilicheza na Chipolopolo ya Zambia na Super Eagles ya Nigeria, katika fainali zilizoandaliwa nchini Libya.

Ethiopia ililazwa tatu bila na Nigeria na moja bila na Zambia na mashabiki wengi wa mpira nje ya kanda ya Afrika Mashariki wanatarajia matokeo kama hayo.

Wachumbuzi wanahisi kuwa nafasi ya kwanza na pili katika kundi hilo zitatwaliwa na Zambia na Nigeria, huku Ethiopia na Burkina Faso zikiwania nafasi ya tatu na nne.

Na ili kufuzu kwa fainali hizo, Vijana hao wa Sewnet Bishaw, waliiondoa timu ya taifa ya Benini katika harakati za kufuzu kabla ya kuwekwka kundi moja na Sudan.

Tumejifunza mengi na tuko tayari asema Bishaw

Bishawa mabaye anaifunza timu hiyo ya The Antelopes kwa mara ya pili, amefanikiwa kubadili mienendo ya baadhi ya raia wa nchi hiyo, ambao walikuwa na tabia ya kutohudhuria mechi za timu ya taifa mwishoni mwa juma na badala yake kutizama mechi za ligi kuu ya mataifa ya England na Uhispania.

Timu ya Taifa ya Ethiopia

Timu ya Taifa ya Ethiopia ikiwasili Afrika Kusini

''Tulijitahidi sana kufuzu kwa fainali na watu ni lazima wafurahie hilo. Tuliwaondoa miamba wa soka kama vile Sudan na Benin, na hatutakuwa timu inayo dharauliwa na wapinzani wetu'' Alisema kocha huyo Bishaw.

Akiongea na wandishi wa habari, Bishaw alisema kuwa bidii ya wachezaji wa wasimamizi wa timu hiyo imezaa mamtunda.

Aliongeza kuwa vijana wake walikuwa na nidhamu ya hali ya juu hali iliyofanya kazi yake kuwa rahisi, ila ameonya wachezaji wake kujifunza zaidi na makosa waliyofanya mjini Khartoum pale walipofunga magoli matano.

Bishaw aliteuliwa kuongoza timu hiyo ya Ethiopia wakati makocha wengi walikuwa wakiisusia, kwa hofu ya kufutwa kazi.

Katika kipini cha miaka kumi iliyopita timu hiyo imefunzwa na makocha kumi na watano akiwemo Iffy Onuora ambaye alifutwa kazi kwa kuwaambia waandishi wa habari kuwa, mara nyingi yeye na wachezaji wake hulazimika kila mara kuwaondoa ngombe uwanjani kabla ya kuanza mazoezi yao.

Lakini katika siku za hivi karibuni, hapajakuwa na tukio lolote la ngombe kupatikana katika viwanja vya michezo nchini Ethiopia ila wachezaji wa soka wa timu hiyo ya taifa.

Hata hivyo idadi kubwa ya wachezaji wa timu hiyo ni kutoka vilabu viwili vikuu vinavyoshiriki katika ligi kuu ya premeir nchini humo vya St. George and Dedebit.

Mshambulizi mmoja wa timu hiyo Saladin Said, anacheza soka ya kulipwa nchini Misri.

Vile vile kuna wachezaji wawili wanaocheza nchini Afrika Kusini.
Mcheza kiungo Yusuf Salah naye anaichezea klabu moja ya Sweden huku Fuad Ibrahim akiichezea klabu moja ya Marekani.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO