Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: SHEREHE ZA 49 ZAMAPINDUZI ZANZIBAR ZILIVYOFANA UWANJA WA AMANI JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani  jini Zanzibar

 

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita kwa ukakamavu mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kutoa heshima kwake na Viongozi wa Juu wa Kiserikali waliohudhuria Maadhimisho ya siku ya mapinduzi Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
zilizofanyika leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.Msanii Halikuniki akiongoza Kikundi cha wasanii cha Cha Beni Maarufu(Mbwakachoka) kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium  jini Zanzibar

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.

 Kikundi cha wasanii cha Mbwakachoka kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.

Baadhi ya wananchi wakipita kwa Maandamano mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama mwanamwema Shein, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, wakiwa katika Jukwa la VIP katika kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar kupitia katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapunduzi Matukufu ya Zanzibar huko Uwanja wa Amaan Studiuma Mjini Zanzibar jana, kuhudhuriwa na Maelfu ya wananchi mbali mbali Mjini na Mashamba.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]

Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikipita mbale ya Rais kwa Gwaride la Mwendo wa kuruka ruka, katika sherehe za Kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matiukufu ya Zanzibar huko
Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar jana. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]

Kikosi cha Jeshi la (KMKM) Kikosi cha kuzuia Magendo Wanaume kikipita mbale ya Rais kwa Gwaride la Mwendo wa haraka, katika sherehe za Kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matiukufu ya Zanzibar huko Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar jana. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu – ZANZIBAR]

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO