Wataalamu wa ujenzi pamoja na wawakilishi wa Shirika la NSSF katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya Jengo kubwa na la kisasa la shirika hilo lililojengwa Jijini Arusha, barabara ya Old Moshi. Jengo hilo lenye jumla ya ghorofa 15, mbili zikiwa chini (basement) kwa ajili ya maegesho ya magari linaelezwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 28.75 na limejengwa kwa muda wa miaka miwili.
Kamapuni ya China Jiangchang Engineering Co. Ltd (CRJE) ndiyo imekabidhi mradi huo ramsi hii leo baada ya kukamilika ujenzi wake uliowashirikisha pia wakandarasi wadogo 6 wa ndani.
Jiji la Arusha limepata muonekano mpya kwa kuongezewa jengo refu, kubwa na la kisasa kwa shughuli za kiosifi na biashara. NSSF nao wanategemea kuhamishia offisi zao kwa kanda hii katika jengo hili, halikadhalika huduma za kibenki zitapatikana hapo.
Sehemu ya mbele ya jengo, upande wa kushoto
Jengo jipya la Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililoko Jijini Arusha, Barabara ya Old Moshi. Jengo hilo limekabidhiwa leo kwa shirika hilo toka kwa mkandarasi kutoka China ambae alishirikiana na wakandarasi wengine wa ndani.
Mkadiriaji na msimamizi wa gaharama za mradi, QS Komba akifafanua jambo kwa mwakilishi wa NSSF, Eng. Mattaka wakati wa ukaguzi wa jengo hilo leo kabla ya makabidhiano ramsi.
Timu ikifanya ukaguzi eneo la kuegesha magari ndani ya jengo hilo
Mbunifu wa jengo, mwakilishi wa NSSF, Injinia Mshauri pamoja na injinia mkaazi wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa maalumu kwa ajili yao na wataalalmu wengine walioshiriki katika ujenzi wa mradi huo, katika hoteli ya kitalii ya Kibo Palace ya Jijini Arusha
Wakandarasi wa kichina pamoja na mkadiriaji majenzi wa mradi, QS Komba wakiwa katika maakuli
Mkadiriaji majenzi wa mradi huo, QS Komba na wataalamu wengine waliofanikisha mradi huo, pamoja na mwakilishi wa NSSF wakiangalia picha za jengo hilo walizopiga hii leo Jijini Arusha
Architect Dudley Mawalla kutoka MD Consultancy Ltd ya Jijini Dar es Salaam (aliyekunja mikono), ambae ndiye mbunifu wa jengo hilo la NSSF Jijini Arusha katika mkutano wa makabidhiano ya mradi baada ya kukamilika kwa matumizi hii leo.
Wataalamu waliofanikisha design na michoro ya jengo hilo, wakandarasi wa kichina pamoja na mwakilishi wa NSSF, Eng Mataaka wakibadilishana mawazo mara baada ya kikao cha makabidhiano ya mradi kutoka kwa mkandarasi kwenda kwa NSSF.
Injinia Mattaka (katikati) kutoka NSSF akipata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa usalama wa jengo hilo namna ambavyo mitambo ya kiusalama imefungwa na inavyofanya kazi.
0 maoni:
Post a Comment