Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji

WATU 12 raia wa Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Singida, kulipa faini ya Sh100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya  Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.

Pia mahakama hiyo, imeamuru basi la Kampuni ya Mtei ya mjini Arusha lililokuwa limebeba Waethiopia hao kukamatwa na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.

Waethiopia hao ambao wote bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud, Tazana  Walao, Mohammed Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abdalah na Alamu Gabresekesie.

Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu  Kidisu, Yassin Mohammed Hassan, Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.

Baada ya mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Ahmed Seif kuwasomea makosa hayo mawili ya kuingia na kuishi  nchini bila ya kuwa na kibali, washtakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa hayo.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mwanasheria wa Serikali, Seif, aliiomba mahakama hiyo  iwape adhabu kali washtakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali chochote halali.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Kiongozi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na upande wa mashtaka na utetezi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa faini ya Sh100,000 kila mshtakiwa.
Washtakiwa wote 12 walilipa faini hiyo.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali Seif, washtakiwa hao walikamatwa Januari 17, mwaka huu alasiri katika eneo la Kijiji cha Kititimo nje kidogo ya Mji wa Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakidai kwenda Afrika Kusini

Imeripotiwa na Gazeti Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO