Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA (AFCON 2013) KUANZA LEO JANUARI 19

Kesho ni Ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwenyeji Afrika Kusini kucheza na timu ya Taifa ya Cape Verde. Mechi nyingine ya ufunguzi itakuwa baina ya Angola na Morocco katika kundi A.

Michuano ya Mataifa ya Afrika imeanza kujulikana kwa kasi hususani na watafiti wa soka ulimwengu kwani wamekuwa wakija Afrika kutafuta vipaji kwa ajili ya kucheza soka barani Ulaya na kwingineko.

Maafisa mbalimbali wa vilabu na timu za mataifa mengine wanaendelea kumiminika kwa ajili ya fainali hizi ikiwa ni mara baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini humo akiwemo kocha Mkuu wa Taifa Stars ambaye ameondoka mapema leo mchana.

Katika kundi A linalofungua leo macho ya watazamaji yatakuwa kwa nyota Youssef El Arabi raia wa Morocco anayechezea Ligi Kuu Hispania katika klabu ya Granada na upande wa Angola akitazamwa Manucho ambaye huchezea klabu ya Real Valladolid ya Hispania.

Kwa wenyeji Afrika Kusini umahiri wa May Mahlangu (23) anayechezea klabu ya Helsingborgs ya nchini Sweden ambapo mwaka 2011 alitajwa kuwa mchezaji bora wa Allsveskan huku Cape Verde macho yakitupiwa kwa nyota Ryan Mendes nyota wa klabu ya Lille ya Ufaransa aliyewaua Kameruni wasishiriki michuano hii mwaka 2013.

Mitanange ya Makundi inaanza hapo kesho Jumamosi Januari 19 na kumalizika Januari 30 mwaka huu.


Stori na Jaiz Malelo, Picha na http://allthingsjabu.co.za/

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO