Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Shule iliyofungwa na Mh Lema juzi yafunguliwa na Mkuu wa Wilaya; Mkuu wa Shule avuliwa cheo

Mh John Mongela, Mkuu wa Wilaya ya Arusha

MKUU wa Wilaya ya Arusha, John Mongela (pichani), ametangaza kuifungua Shule ya Sekondari Korona iliyopo Njiro kwa Msolwa ambayo juzi ilifungwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi likiwamo tatizo la usafiri na ukosefu wa miundombinu.

Pamoja na uamuazi huo, mkuu huyo wa wilaya jana alitangaza kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo, John Mbise, ambaye hakuwapo shuleni hapo licha ya kupewa taarifa za ugeni huo.

Aidha, amemuagiza Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji, Violet Kiwowoza, hadi jana majira ya saa sita awe amewasilisha barua ya kutenguliwa cheo kwa mkuu huyo wa shule ofisini kwake na awe amebandika matokeo ya kidato cha pili shuleni hapo.

Pia amemuagiza mkurugenzi kuwasilisha mchanganuo wa shule hiyo kuwa ya bweni. Alisema ameifungua shule hiyo kwa kuwa Lema hakufuata taratibu za kuifunga, lakini alikiri kuwa shule hiyo ina matatizo mengi ambayo alisema kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na uzembe wa watendaji na viongozi wa Idara ya Elimu.

“Tusiigeuze hoja hii kama ni matatizo ya mbunge na kuleta siasa, lakini ni wajibu kuwajibishana watendaji kutokana na uzembe, hata maji yamekatwa eti kwa kushindwa kulipa bili ya sh 300,000. Hii ni aibu kwa jiji, wakaguzi wa elimu siku zote walikuwa wapi hadi haya yote yanatokea?’’ alihoji Mongela.

Mongela aliwatahadharisha watendaji wa serikali kuwa wasishangae siku za usoni kumuona akiungana na Mbunge Lema katika kushinikiza baadhi ya mambo kufanyika kwa ufanisi kama inavyohitajika.

“Mimi nadhani japo wengine wanachukia Lema kushinda kesi yake, lakini nadhani Mungu ndiye alipanga hivyo, ili aje kufichua mambo haya, kwani sisi japo tungeyabaini lakini ingechukua muda mwingi,’’ alisema Mongela.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake baada ya uamuzi wa mkuu wa wilaya, Mbunge Lema alisema yeye kama mbunge alikuwa anatambua kuwa sheria hazimruhusu kufanya hivyo, lakini kama mtetezi wa wananchi wa Arusha alilazimika kuchukua uamuzi huo ili kuwasaidia wanafunzi ambao kwa wiki tatu sasa hawapati masomo na wana shida ya usafiri na matatizo ya maji.

na Ramadhani Siwayombe, Tanzania Daima - Arusha

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO