Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wakuu 3 wa Polisi wafutwa kazi Kenya

Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe anayedaiwa kuwa na uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu

Maafisa watatu waandamizi wa polisi nchini Kenya, wamesimamishwa kazi kuhusiana na sakata ya mtu mmoja ambaye aliwalaghai watu kuwa yeye ni naibu kamishna mkuu wa polisi kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe anayedaiwa kuwa na uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu ni mmoja wa wale waliofutwa kazi.

Taarifa zinazohusiana

Mwenyekiti wa tume ya kuwaajiri maafisa wa polisi KPSC Johnstone Kavulundi, amesema maafisa hao watatu wametajwa kuhusika kwa njia moja au nyingine na kashfa hiyo.

Wiki iliyopita, Joshua Waiganjo, alifikishwa mahakamani, kwa kujifanya afisa mwandamizi wa polisi katika mkoa wa Rift Valley.

Mshukiwa huyo amekanusha madai hayo.

Ripoti zinasema kuwa ulaghai huo ulifichuliwa, wakati aliposafiri kwa ndege ya polisi, kwenda kuchunguza mauaji wa maafisa 42 wa polisi waliouawa na wezi wa ng'ombe katika bonde la Suguta, tukio ambalo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.

Rais Mwai Kibaki ameagiza uchunguzi kamili kuhusiana na tukio hilo.

Bwana Kavulundi amesema kuwa mkuu wa polisi mkoani humo John M'Mbijiwe, afisa mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na wezi wa mifugo ASTU Remi Ngugi na afisa mkuu wa polisi wilayani Njoro Peter Nthiga wamesimamishwa kazi.

Amesema watatu hao huenda wakahujumu uchunguzi ikiwa wataendelea kusalia madarakani.

Joshua Waiganjo amesemekana kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wengine wa polisi katika mkoa wa Rift Valley wakati huo.

Baada ya kukana mashtaka hayo, kesi hiyo ilihairishwa ili kumruhusu mshukiwa huyo kutafuta matibabu kutokana na ugonjwa wa kisukari katika hospitali moja nchini humo.

Chanzo: BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO