Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HOT POTS ZATUMIKA KUINGIZA SIMU MAGEREZANI

Afisa wa Magereza wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonyesha mfuniko wa Hotpot (Chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo vinatumika kuficha simu, visu, bangi na vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa Mahabusu na wafungwa. Vifaa hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao pmaoja na baadhi ya ndugu zao wanapopeleka chakula gerezani hapo. Hata hivyo, maafisa magereza kwa kutumia chombo cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo huvikamata vifaa hivyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa

CHANZO: JAIZMELALEO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO