Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Umoja wa Wafanyabiashara wa Oman Kutumia Sh160 bilioni Kufufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)

Na Fredy Azzah 


UMOJA wa wafanyabiashara wa Oman, upo katika mchakato wa kukamilisha uwekezaji wa Sh160 bilioni katika Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lusajo, zinaeleza kuwa fedha hizo zinatarajiwa kuingizwa katika kampuni hiyo katika kipindi cha miezi sita hadi 10 ijayo.

Kapteni Lusajo alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika katika ununuzi wa ndege, ukodishaji na shughuli nyingine za kuliendesha shirika hilo.

Alisema ujumbe huo umeshakuja nchini kufanya mazungumzo ya awali na kwamba utarudi kwa awamu ya pili kujadili mkataba huo wa uwekezaji.
Alisema hivi karibuni mwenyekiti wa wafanyabiashara hao alifika nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya awali.

“Rais alienda Oman kufanya ziara, alikutana na wafanyabiashara wa huko na walionyesha nia ya kuja kuwekeza huku kwetu na kweli hivi karibuni mwenyekiti wao alikuja,” alisema.
Kapteni Lusajo alisema wafanyabiashara hao watakuja kufanya uwekezaji wa jumla katika shirika hilo, ikiwamo kutoa mafunzo.

“Tulichofanya mpaka sasa ni mazungumzo ya awali, siwezi kueleza kiundani sisi tunanufaika vipi na wao watanufaika vipi, tunasubiri warudi na barua ya kuomba kufanya uwekezaji huo ambayo ndiyo itakuwa imebainisha kila kitu kwa undani na hapo ndio tutaanza kujadiliana,” alieleza.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Sheikh Salim Al Harthy alisema kufanya uwekezaji huo wa dola za Marekani 100 milioni, kutaongeza uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
Taarifa ya Mwenyekiti huyo iliyopatikana jijini Dar es Salaam jana inaeleza kuwa uwekezaji huo utahusisha kukodisha na kununua ndege ambazo zitatumika katika safari za ndani ya Tanzania na nje.
“Mpango wetu ni kujenga kituo cha mafunzo ya masuala ya ndege, ofisi nzuri kwa ajili ya ATCL, kununua ndege na kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Tunatarajia kufanya haya katika kipindi cha kuanzia miezi sita hadi kumi ijayo,” alisema.

Taarifa kutoka Oman zinaeleza kuwa, mbali na wafanyabiashara hao waliokuja kuwekeza kwenye usafiri wa anga, makundi mengine yanatarajiwa kuja kujikita katika sekta ya mafuta.

Hayo yalielezwa katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Oman lililofanyika Oktoba 16 nchini humo ambako Rais Kikwete alitoa hotuba.
Kongamano hilo liliangalia fursa za kibiashara zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kwenye sekta ya kilimo, viwanda, utalii, usafirishaji mafuta na gesi.

Kituo cha Uwekezaji (TIC), kiliwasilisha fursa mbalimbali za uwekezaji na namna ya kuweza kuzipata.

Kwa nyakati tofauti ATCL ilibinafsishwa bila kuleta matunda na katika awamu zote hizo, shirika hilo limeendelea kupata hasara.

Licha ya shirika hilo kubinafsishwa kwa Afrika Kusini bila matunda kuonekana, pia Serikali kuu imekuwa ikitoa fedha za kuendesha shirika hilo bila mafanikio.

Chanzo: Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO