Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DJ NA MTANGAZAJI WA MJ RADIO 93.0 FM YA JIJINI ARUSHA AELEZWA KUFARIKI DUNIA

Dj Bupe enzi za uhai wake akiwajibika
*********

Taarifa iliyoandikwa na Blog ya Dj Haazu ya Jijini hapa inayomilikiwa na Dj Haazu ambae pia ni Dj na Mtangazaji katika redio hiyo, inaeleza kuwa Mtangazaji mwenzao Samorina Ambakisye ama Dj Bupe amefariki dunia jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu!

”KIUKWELI NI NGUMUKUAMINI ILA UKWELI NI KWAMBA MTANGAZAJI MWENZETU NA DJ SAMORINA AMBAKISYE a.k.a DJ BUPE  HATUKO NAYE TENA DUNIANI AMETUTOKA LEO MCHANA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU

MUNGU AMEMPENDA ZAIDI JAPO TULIMPENDA SANA DJ BUPE...... INNALLAH WAINALLAH RAJIUN.... MUNGU AILAZE ROHO YA DJ BUPE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN...
TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI NA TUTAENZI NA KUFUATA UTU, MAPENZI YAKO NA SUPPORT ULIYOKUWA UNAITOA KWA MZIKI WA NYUMBANI ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Marehemu Samorina anaelezwa kuwa alikuwa akifanya kazi Mambo Jambo Redio kama Dj na pia mtangazaji na kati ya vipindi alivyokuwa akifanya ni pamoja na:

** Dance Fever (kila Ijumaa saa moja hadi  saa sita usiku)
** Reggae Fever (kila Jumapili kuanzia saa tisa hadi saa kumi na mbili jioni) na,

** Night Express

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO