Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge Basi la abiria la 'Bunda express" lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza muda wa saa mbili asubuhi hii limepata ajali mbaya kwenye eneo hilo.
Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.
Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri.
Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao.
Mpaka tunaenda mitamboni idadi ya watu waliopoteza maisha ni wawili na 36 majeruhi,
Watu 24 waliopata majeraha makubwa wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza Na majeruhi 12 wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Magu. Chanzo cha ajali kinatajwa kuwa ni mwendo kasi wa busi hilo.
Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.
PICHA ZAIDI UNGANA NA G SENGO HAPA
0 maoni:
Post a Comment