Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha wakiharibu madawa ya kulevya aina ya mirungi iliyokamatwa leo asubuhi eneo la Engikareti Wilayani Longido, Arusha baada ya msaada mkubwa wa taarifa kutoka kwa raia wema. Gari iliyokamatwa na mirungi hiyo ni aina ya Mitsubish Canter, lenye namba za usajili T 306 BUN gari ambalo pia lina kesi nyingine mahakamani kutokana na kukamatwa Machi 16, mwaka 2012 likiwa pia na shehena ya mirungi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukamata madawa hayo aina ya mirungi iliyokuwa imehifadhiwa kwenye viroba zaidi ya 200 viliyokuwa vinasafirishwa kuingia nchini kutokea nchini Kenya.
Kamanda Sabas, alisema hadi sasa wanawashikilia watu wanne waliosafisha mirungi hiyo. Aliwataja waliokamatwa kuwa ni wakazi wa Oldonyosambu Arumeru, Joel Lukumay, Mussa Mollel, mkazi wa Sombetini Arusha, Rahimu Gilla na mkazi wa Ngaramtoni, Ibrahimu Katambweli.
Gharama halisi za mirungi hiyo haikuweza kufahamika mara moja lakini kwa uzoefu inakadiriwa kufikia Sh milioni 30.
Gari iliyokamatwa na mzigo huo ukiwa umechanganywa na piki piki
0 maoni:
Post a Comment