Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MCHINA AKAMATWA KWA KUMPA DC RUSHWA YA LAKI TANO APATIWE TENDA YA KUSAMBAZA PEMBEJEO

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe

Na. George Marato - Mara

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU katika wilaya ya Bunda mkoani Mara imemkamata raia mmoja wa nchi ya China wakati akitoa rushwa ya shilingi laki tano kwa mkuu wa wilaya ya Bunda ili kampuni yake iruhusiwe kusambaza pembejeo kwa wakulima wilayani humo.

Raia huyo wa china Bw. Mark Wang Wei ni mkurugenzi wa kampuni ya Panda International LTD ya mkoani Shinyanga ambaye amekamatwa jana jumatano mchana katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda hiyo Bw Joshua Mirumbe baada ya mkuu huyo wa wilaya kuweka mtego huo wa Takukuru.

Akisimulia tukio hilo mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo,amesema kuwa raia huyo wan chi ya China kupitia kampuni yake alimwandikia ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi akimshukuru sana huku akiaidi kumuona ofisini kwake ili ampe zawadi yake.

Bw. Mirumbe amesema kuwa baada ya kuaidiwa na raia huyo wa china amesema ilimtia shaka kupita kiasi kwa vile hawakuwa na ahadi yoyote kutoka kwake na ndipo akaamua kuwataarifu Takukuru ambao waliweka mtego kwa kuzunguka ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya.

Amesema baada ya raia huyo kuingia ofisini kwa mkuu wa wilaya na kumpa barua kutoka Uhamiaji ikimtambulisha kuwa anacho kibali cha kuishi hapa nchini hadi mwezi wa tatu mwaka huu,raia huyo china pia alitoa kiasi cha shilingi laki tano na kumpa huku akisema kuwa hiyo ni zawadi yake ili airuhusu kampuni yake iweze kusambaza pembejeo kwa wakulima wilayani humo.

Amesema kutokana na wasambazaji wa pembejeo wa wilaya ya Bunda katika msimu wa mwaka jana kuchakachua pembejeo hizo na kusababisha wakulima kuzikosa jambo ambalo limewafanya msimu wa mwaka huu kuwa makini katika kupokea mawakala ambao wamekuwa wakitumia rushwa kupata kazi hiyo kwa lengo la kuhujumu juhudi za serikali katika kuwawezesha wakulima.

Hata hivyo baada ya kutoa fedha hizo PCCB walimtaka kuhesabiwa mbele ya mashahidi akiwa ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ambapo hadi leo bado alikuwa akiendelea kuhojiwa na PCCB, ambao wamesema kuwa baada ya maelezo yake watamfikisha mahakamani kwa kosa la kutoa rushwa.

Akihojiwa na waandishi wa habari raia huyo wa china Bw Mark Wang Weiamekiri kutoa pesa hizo huku akisema alimpa mkuu huyo wa wilaya kama zawadi yake na kwamba wala hiyo siyo rushwa.

Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Bunda, Bw.Masuke Ogwa, amewaambia wandishi wa habari kuwa kampuni hiyo ya china ilikuwa bado haijaruhusiwa kusambaza pembejeo wilayani humo, kutokana na kutokuwa na vielelezo vinavyotakiwa vya kumruhusu kuwa hapa nchini.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO