Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM Zanzibar yataka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea urais wa visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara.

 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai-

--

Na: Elias Msuya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kimeeleza nia yake ya kutaka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea urais wa visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara. Pamoja na hatua hiyo, chama hicho pia kinafikiria kurejea mtindo wa kupokezana kiti cha urais wa Tanzania kati ya bara na visiwani kama ilivyokuwa awali, ili kuweka usawa katika Muungano.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikazua mpasuko na malumbano mapya kuhusu suala la urais ndani ya CCM, ambako harakati za baadhi ya wanachama wake wameanza kupiga mbio za kuutaka urais katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Akizungumza katika mahojiano maalumu visiwani humo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, alisema kwa sasa suala hilo linajadiliwa na kwamba ana matumaini kuwa litapatiwa ufumbuzi.

Hatua hiyo imekuja wakati Zanzibar ikiadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi yaliyoung’oa madarakani utawala wa mabavu wa Sultani, huku ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani, utakaofanyika 2015.

“Ndani ya CCM tuna utaratibu wetu wa kupata viongozi, lakini hilo suala la kuchaguliwa mgombea urais kutoka kwenye vikao vya Dodoma hata sisi limetugusa... Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kulijadili ili tupate ufumbuzi,” alisema Vuai na kuongeza:

“Siyo tu kuchaguliwa mgombea urais, hata suala la kupokezana urais na jinsi ya kupata viongozi wengine kama wabunge na wawakilishi tunalijadili kwa kina. Ninaamini tutapata ufumbuzi… Siwezi kusema lini kwa kuwa chama chetu ni kikubwa mno, lakini tunalijadili.”

Vuai ametoa kauli hiyo, huku kukiwa na malalamiko ya Wazanzibari wengi kuhusu Muungano, ambapo wengine wanahoji iwapo kuna haja ya kuendelea na utaratibu wa sasa kupata mgombea na Rais wa Zanzibar ambao ni lazima upate baraka za CCM Bara.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema jambo hilo halijafikishwa kwenye vikao rasmi vya chama.

“Kama wao wanalifikiria hilo, acha waendelee, labda ungewauliza kama wameshalifikisha kwetu. Ukiniuliza mimi nitakujibu kuhusu utaratibu tulionao sasa, ila kama wao wana hoja nyingine, basi watazileta kwenye vikao husika zitajadiliwa,” alisema Nape.

Naye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, akizungumzia suala hilo alisema hayo ni maoni tu ya wananchi na wala Serikali haiwezi kuyaingilia.

“Wazanzibari wana haki ya kutoa maoni yao na wala Serikali hatuyaingilii. Lakini waelewe kwamba bado Muungano una faida kubwa kwetu. Hapa kwetu uchumi ni mdogo, ardhi ni ndogo pia Zanzibar inapata ulinzi na usalama kutoka kwenye Muungano,” alisema Waziri Aboud.

Mapinduzi na Muungano
Akizungumzia mafanikio ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vuai alipinga madai kuwa Mapinduzi hayo yamemezwa na Serikali ya Muungano.“Nakubali kuwa Mapinduzi yalilenga kuikomboa Zanzibar ili iwe huru, lakini siamini kama Zanzibar imemezwa na Muungano.,” alisema Vuai.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO